Pages

Wednesday, May 15, 2013

"MWANGA WAONEKANA SASA KATIKA SANAA YA MUZIKI" - ZITTO KABWE.


Mhe. Zitto Kabwe

Baada ya malalamiko ya muda mrefu sana kuhusu wanamuziki kutofaidika na biashara ya miito ya simu (ring back tones - #RBT), hatimaye Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdallah Kigoda ameagiza #COSOTA kufanya marekebisho ya kanuni ili kuweka kiwango cha mrabaha Kwa wasanii kutoka pato ghafi la biashara hiyo Kwa kampuni za simu. 


Vile vile kanuni namba 3 ya Kanuni za Sheria ya Hakimiliki, Sheria namba 7 ya mwaka 1999 itaanza kutumika rasmi na hivyo wasanii kulipwa mrabaha kutokana na nyimbo zao kupigwa kwenye vituo vya redio na televisheni. 


Agizo hili la Waziri Kigoda linavunjilia mbali mfumo wa kinyonyaji uliokuwa unafanywa na kampuni za simu Kwa kuuza kazi za wasanii bila mikataba na kujiamulia wenyewe Kiwango Cha malipo. Uamuzi huu Ni ukombozi Kwa wasanii wetu. 


Watumie mapato haya makubwa watakayopata kuwekeza kwenye kuboresha kazi zao na kuwa na uwezo wa kuingia mikataba bora zaidi Kwa kuajiri wanasheria mahiri. Shime wasanii wetu, kazi kwenu!

No comments:

Post a Comment