Pages

Friday, May 17, 2013

UKATILI: MLINZI WA BAA ACHINJWA KAMA KUKU NA MAJAMBAZI USIKU WA KUAMKIA LEO HUKO KIMARA STOP OVER....ANGALIA PICHA ZA TUKIO HILO

 

     Sehemu aliyochinjiwa mlini huyo aliyefahamika kwa jina Mika Athumani.
 Mwananachi akishuhudia damu ya mlinzi huyo kwa hudhuni
 Baskeli ya Mlizni huyo ikiwa imetapakaa damu ambapo inadaiwa mlinzi huyo alikuwa amelala kwenye eneo hilo
     Redio ambayo majambazi hayo waliiangusha nje ya baa hiyo
 Askali kanzu aliyefahamika kwa jina la Sunzu akipiga picha sehemu ya mlango ambayo majambazi hayo yalivunja na kuingia ndani muda mfupi baada ya kumchinja mlini huyo
 Majaira ya saa 12 asubuhi ya leo wananchi walishuhudia maduka mawili ya baa hiyo yakiwa wazi huku mwili wa mlizni huyo umekutwa upande wa baa ukiwa umechinjwa na kutenganishwa kichwa na mwili
                 Umati wa watu ukishuhudia tukio hilo muda mfupi uliopita










              Gali la polisi likiondoka eneo la tukio na mwili wa marehemu


                        Wananchi nao waliondoka eneo hilo la tukio
 Mmili wa baa hiyo Bw Salvatory Mushi akihojiwa na waandishi wa habari eneo la tukio
            Majirani wa eneo hilo wakihojiwa na waandishi wa habari
                              
MLINZI wa baa ya Darajani Stop Over iliyo kando kando ya barabara kuu ya Morogoro=Dar es salaam jirani na daraja la Mzambarauni mkoani hapa Bw Mika Athumani  amechinjwa na majambazi usiku wa kuamkia leo.
Habari zilizoptaikana eneo la tukio zilidai kwamba majambao hao baada ya kuvamia baa hiyo iliyojitenga usiku wa manane  na kumvamia mlinzi huyo na kumchinka kama kuku na baadae kuvunja baa hiyo na kuimba vitu mbali mbali.
Akihojiwa na Mtandao huu mmiliki wa baa hiyo Bw Salvatory Mushi alidai kwamba majambao hao walimvamia mlinzi wake na kumchionja bna baadae walivunja Counter ya baa hiyo pamoja na duka ililipojirani na baa hiyo na kuiba vitu mbali mbali.
Alipoulizwa kwamba kuna taarifa zinadai kwamba mlinzi huyo alikutwa akiwa amelala Bw Mushi alisema" inawezekana lakini hakuna mtu mwenye uhakika na jambo hilo kwani sote hatukuwepo,wakti tukio hilo linatokea"alisema Bw Mushi ambaye anadai bado hajafahami dhamani ya vitu vilivyoibikiwa na majambazi hayo.

 
 Mwili wa marehemu ukiwa ndani ya gari, la polisi kufuatia mwili huo kutenganiswa vibande viwili mtandao huu umesita kuweka picha hiyo


Baadhi ya watu waliokuwepo eneo hilo la tukio walidai kwamba mlinzi huyo alikuwa amelala hivyo majambazi hayo yalimvamia na kumpora siraha zake na kishi kumchinja shingoni," siumeona alikuwa amelala jirani na baiskeli yake ndio maana ameshindwa kupamabna nao hasa ukizingatia baa hii imejitenga iko peke yake hapa jirani na mto wa Morogoro"alisema Bw Maneo Mashani.
Mtandao huu ulishuhudia mtoto wa marehemu pamoja na mjukuu wa marehemu wakiangua vilio eneo la tuko baada ya kuuona mwili wa mazazi wao aliyeuwawa kikatili baadae wote wawili walipanda gari la polisi na kuondoka nao.

No comments:

Post a Comment