Pages

Thursday, May 16, 2013

VIVUTIO NYANDA ZA JUU KUSINI KUTANGAZWA

 

 

SERIKALI imesema ipo katika mchakato wa kuvitangaza vivutio vya utalii vilivyopo Nyanda za Juu Kusini.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Ofisa Habari wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Tulizo Kilaga, alisema mkoa mmojawapo ambao bado hautambuliki katika sekta ya utalii ni Mbeya, ambayo ina vivutio vya aina yake.

Alisema hawatangazi vivutio hivyo kwa watalii kutoka nje pekee, bali hata Watanzania ambao ndio wamiliki wa rasilimali asili wanatakiwa kuvifahamu na kuvitembelea.

Alisema Watanzania wakiwa na tabia ya kutembelea vivutio vilivyopo nchini, watapanua ufahamu wa elimu na kuongeza uzalendo.

Alilitaja Ziwa Ngozi kama mojawapo ya kivutio kikubwa ambacho si tu kinavutia kutembelea, bali pia kina historia ya pekee.

Tulizo alisema ziwa hilo lililopo kati ya Wilaya ya Mbeya na Rungwe, limezungukwa na milima, ukiwemo Mlima Ngozi.

Akizungumza na waandishi wa habari, mmoja wa waongozaji wageni wanaofika katika eneo hilo, Said Jaffar, alisema wamekuwa wakifaidika na ziwa hilo, ambapo pia ni sehemu ya ajira kwa vijana waishio katika eneo hilo.

“Msimu wa kiangazi, huwa tunapata wageni wengi hasa wanafunzi, ila natumai likitangazwa vizuri, idadi ya watalii itaongezeka,” alisema.

Wakazi wa eneo ilo walisema ziwa hilo limekuwa halijai maji wala kupungua kwa majira yote ya mwaka.

No comments:

Post a Comment