Pages

Saturday, May 18, 2013

WAJUE Wasandawe

 

Wasandawe ni kabila linaloishi hasa katika eneo la wilaya ya Kondoa, mkoa wa Dodoma, katikati ya nchi ya Tanzania.

Wasandawe katika wilaya ya Kondoa wanaishi hasa katika tarafa mbili, yaani Farkwa na Kwamtoro. Kabila hilo la pekee linaonekana katika vipimo kuwa na viini nasaba vya zamani kuliko makabila yote duniani.

Ndugu zao wa jirani ni hasa Wakhoisan wa Kusini mwa Afrika, halafu Waethiopia.

Mwaka 2000 idadi ya Wasandawe ilikadiriwa kuwa 40,000 , wengi wao wakiwa Wakristo, hasa Wakatoliki.

Lugha yao ni Kisandawe, ya jamii ya Kikhoisan, ina fonimu nyingi kuliko lugha zote duniani, zikiwa ni pamoja na "click sounds". Inafikiriwa kuwa ya zamani kuliko zote, kwa kuwa inafanana bado na zile za wenzao Kusini mwa Afrika, ingawa walitengana miaka 40,000 hivi iliyopita.

Miaka ya nyuma wengi wao walikuwa hawajasoma bali sasa wanasomesha vijana wao, hasa baada ya kuanzishwa shule za kata kama Farkwa Secondary, Kwamtoro Secondary, Makarongo Secondary, Gwandi Secondary, Kurio Secondary n.k.

Vilevile Wasandawe wameanza kujihusisha na kilimo japo bado wanaendelea na uwindaji.

Jamani kama kuna mtu yeyote anafahamu chochote juu ya wasandawe anitumie kupitia icehabari@gmail.com

No comments:

Post a Comment