Pages

Saturday, May 18, 2013

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI, MHE. PEREIRA AME SILIMA AZINDUA HUDUMA ZA DUTY FREE SHOPS KATIKA JESHI LA MAGEREZA, MJINI DODOMA.


 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Supermarket (Duty Free Shop) ya pili ya Jeshi la Magereza iliyojengwa katika Mkoa wa Dodoma.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Military Shop, Afzal Meghji akimuonyesha bidhaa mbalimbali zilizopo ndani ya Duty Free Shop ya Jeshi la Magereza, Isanga mkoani Dodoma, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (kulia). Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, John Minja.
 Baadhi ya maafisa na askari Magereza wakinunua bidhaa mbalimbali baada ya kuzinduliwa kwa Supermakert (Duty Free Shop) ya Jeshi la Magereza iliyopo Isanga, mjini Dodoma.
 Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja akitoa hotuba fupi ya kumkaribisha mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima kufungua Supermarket (Duty Free Shop) ya pili ya kisasa ambayo imejengwa na jeshi hilo, katika Gereza Isanga, mjini Dodoma. Ufunguzi huo umefanyika leo mjini humo.

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akizungumza na maafisa magereza kabla ya kufungua Supermarket (Duty Free Shop) ya pili ya kisasa ya Jeshi la Magereza ambayo itawawezesha maafisa wa jeshi hilo, askari na familia zao kupata huduma ya kununua bidhaa mbalimbali kwa bei nafuu. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, John Minja na kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Military Shops ambaye ndiye aliyewekeza katika Supermarket hiyo, Afzal Meghji. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (wa katikati waliokaa), Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, John Minja, (wa tatu kushoto waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa mbalimbali wa magereza pamoja na wageni waalikwa baada ya kufungua Supermarket (Duty Free Shop) ya kisasa ya jeshi hilo, mjini Dodoma.
PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

No comments:

Post a Comment