Pages

Saturday, May 18, 2013

unafahamu kabila la Waburunge?


 Waburunge ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Dodoma, Wilaya ya Kondoa. Lugha yao ni Kiburunge.

Waburunge kwa idadi ni wachache sana na wanapatikana wilaya ya kondoa katika tarafa za Goima na Mondo pia wachache wapo katika kata za Gwandi na Kondoa Mjini.

Waburunge wana tamaduni zifuatazo
1.wanakeketa wanawake hadi leo
2.wanarithi wajane hadi leo,
3.wanaume wanatahiriwa porini na anakaa porini kwa zaidi ya miezi sita
4.ktk suala la ndoa mwanamke hana sauti kwani anaweza kuozeshwa hata mtu asiyemju wala kumuona hata siku moja kwani anasikiliza anachoambiwa na wazazi wake
5.kwa waburunge mwanamke ni kiumbe duni ambaye hana kauli yoyote ile mbele ya wanaume
6.suala la dini kwao ni geni sana kwani dini zimeingia hivi karibuni na hadi sasa robo ya waburunge ni wapagani bali wachache wamejiunga na ukristo na wachache sana wapo katika uislamu
7.suala la elimu kwao ni sumu kwani huona kumpeleka mtoto shule ni sawa na kupoteza muda kwani huwadharau wale wachache ambao wanasomesha na hii imeanza kufutika baada ya serikali kuanzisha shule za kata na kufanya ulazima wa mtoto yeyote yule anayefaulu anatakiwa kwenda shule kwa ulazima kwani wazazi hawapendi.
8.lugha yao ni kiburunge ni ngumu sana kwani si ya kibantu ila ina uhusiano kidogo na lugha za wairaq na wagorowa kwani mburunge anaweza kuelewa mwiraq anachokiongea kutokana na maneno yao kuwa na mizizi ile ile bali viambishi tofauti
9.wana ngoma zao za asili na wanaziheshimu sana kwani kila mtu anachezeshwa kutokana na jinsia yake na kanuni za ukoo lkn kila mtu lazima acheze kwa mwaka ngoma yao kuu hufanyika mwezi wa saba kuanzia tarehe saba hadi kumi katika kijiji cha chambalo.
10 wao wanaamini pombe kama ni kitu cha umuhimu kwani katika shughuli zozote za mkusanyiko lazima pombe iwepo.
11 wanafuga na kuwinda pia
12.wanapenda kukaa milimani sana
13.wana njia zao za asili za kutambua majira ya mwaka na jinsi mwaka utakavyokuwa kama utakuwa na mvua nyingi au kidogo.
14.wana njia za asili za kuhifadhi vyakula.
15.wana vyumba zao za asili ambazo zinajengwa kwa miti na udongo tu.

anayeweza kuniongezea juu ya kabila hili aniandikie kupitia icehabari@gmail.com

1 comment:

  1. ...sijafurahishwa natamaduni zao, hasa inayohusu jinsia ya like!

    ReplyDelete