Pages

Tuesday, May 7, 2013

CCM kata ya Mirerani wamsimamisha katibu kwa madai ya kutoa siri

Halmashauri Kuu ya CCM, Kata ya Endiamtu, Mji mdogo wa Mirerani, wilayani Simanjiro Manyara imeridhia kusimamishwa uongozi wa Katibu wa CCM wa kata hiyo Salim Mohamed kutokana na kutoa nje siri za vikao vyao.

Badala yake, halmashauri hiyo imemteua Katibu wa Jumuiya ya wazazi ya kata hiyo, Isaya Abayo kuwa Kaimu Katibu wa CCM wa kata hiyo, wakati huu ambapo Mohamed amesimamishwa uongozi.

Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho walidai kuwa, wamemsimamisha uongozi katibu huyo kwani ana kawaida ya kutoa nje siri mbalimbali za vikao vyao ikiwamo mikakati ya kukiimarisha chama hicho kiuchumi.

Walisema wenyewe ndiyo waliompa kazi hiyo ya ukatibu wa CCM, Kata ya Endiamtu hivyo wanamsimamisha, pia walishangazwa na kitendo chake cha kuandika barua wilayani aliposimamishwa ilhali angepaswa kuwaandikia wao. (Joseph Lyimo)


No comments:

Post a Comment