Pages

Sunday, May 12, 2013

Dododma: Clouds Media Group yazindua msimu wake mpya kwa kishindo



Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh Zitto Kabwe ambae pia ni mdau kubwa wa Muziki hapa chnini,pia alikuwa ni mmoja wa wazungumzaji kwenye semini hiyo iliyohusu na  harakati rasmi za vita dhidi ya uharamia wa kazi za wasanii,iliyofanyika mapema leo kwenye ukumbi wa hoteli ya African Dreams,nje kidogo ya mji wa Dodoma.kutakuwepo na kampeni ya matembezi ya hisani ya harakati rasmi za vita dhidi ya uharamia wa kazi za wasanii yatakayofanyika kesho,wabunifu na wavumbuzi mbalimbali, mseto wa shuguli mbalimbali zitahusishwa.  Aidha pia mchana huu kutakuwepo na burudani hadhara ya sanaa za kisasa na za kitamaduni,mpira, chakula na bidhaa mbalimbali za kitanzania katika uwanja wa jamhuri .
 Mmoja wa wasemaji kwenye semina hiyo aliyejitambulisha kwa jina la   Patrick Ngowi  kutoka kampuni ya Helvetic Solar Contractors, akizungumzia fursa mbalimbali kuhusiana na mambo ya ujasiliamali na pia alielezea ni namna gani amefanikiwa mpaka kufikia kumilimiki lampuni yake binafsi kupitia fursa alizokuwa akikumna na nazo na kuzifanyia kazi vilivyo. 
 Mmoja wa washiriki wa semina hiyo akiuliza swali kwa Mh Zitto Kabwa kuhusiana na mambo mbalimbali ya ujasiliamali na namna ya kuzitumia fursa hizo katika kujikwamua kimaisha.
 Mh Zitto kabwe akimsikiliza mmoja wa washiriki wa semina hiyo alipokuwa akiulizwa kuhusiana na suala la fursa zinazopatikana kwa vijana na namna ya kuzitumia katika ujumla wa kujikwamua na ugumu maisha,ambapo watanzania wengi wamekuwa wakizilalamikia.



Mtangazaji wa clouds FM kupitia kipindi cha Power Breakfast-Gerald Hando akiikaribisha Meza kuu pamoja na wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye uzinduzi wa msimu mpya wa Clouds Media Group unaokwenda sambamba na ujumbe wao thabiti kabisa  ulioitwa MADE IN TANZANIA,ikiwa na hamasa kubwa ya kuleta msingi wa fursa kwa watanzania, msukumo ikiwa ni kuwashawishi watanzania kuanza kuzifanyia kazi
fursa hizi kwa umoja na maendeleo ambapo TWENZETU, inakuwa neno rasmi la
mawasiliano.Kama vile haitoshi kutakuwepo na kampeni ya matembezi ya hisani ya harakati rasmi za vita dhidi ya uharamia
wa kazi za wasanii yatakayofanyika kesho,wabunifu na wavumbuzi mbalimbali, mseto wa shuguli mbalimbali
zitahusishwa  ikiwemo semina ya fursa kwa
watanzania,burudani hadhara ya sanaa za kisasa na za kitamaduni,mpira, chakula
na bidhaa mbalimbali za kitanzania zitapatikana uwanja wa jamhuri mapema leo mchana.

Mmoja wa wasemaji kwenye semina hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Zenno  Ngowi kutoka kampuni ya Tanzania Home Expo akizungumzia fursa mbalimbali kuhusiana na mambo ya ardhi,ujenzi,na mengineyo mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria kwenye semina hiyo leo mjini Dodoma.





Mmoja wa wasanii mahiri wa Mashairi,Mrisho Mpoto akifafanua jambo kuhusiana na mambo mbalimbali katika suala zima la wasanii kujipa nafasi ya Fursa mbalimbali zinazojitokeza mbele yao na namna ya kuzifanyia kazi na kuziboresha zaidi.
Mhe Zitto Kabwe akiwasili kwenye semina hiyo mapema leo,ambaye pia alikuwa ni mmoja wa wasemaji wa semina hiyo.
Pichani ni washiriki wa semina hiyo kutoka sehemu mbalimbali mjini Dodoma leo.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia jambo kwenye semena iliyokuwa ikiendelea mapem leo kwenye hoteli ya African Dreamz,nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Mtangazaji wa Clouds FM,Loveness Love a.k.a Diva akijitambulisha kwenye semina hiyo
Mtangazaji wa Clouds FM,Shaffih Dauda akijitambulisha kwenye semina hiyo.
wadau wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye semina hiyo iliyoibua changamoto nyingi.
Kutoka Clouds FM,Millard Ayo,Dina Marios pamoja na Zamarad wakifuatilia jambo
Mtangazaji wa Clouds FM,Arnold Kayanda Diva akijitambulisha mbele ya washiriki waliofika kwenye semina hiyo.
Baadhi ya wasanii wakiwa ndani ya semina hiyo katika harakati rasmi za vita dhidi ya uharamia wa kazi zao,ambapo matembezi ya hisani yamepangwa kufanyika kesho na Waziri Mkuu Mh.Pinda anatarajiwa kuyapokea matembezi hayo.
Msanii Afande Sele na Msanii mwenzake wakiwa ndani ya semina hiyo wakifuatilia yaliyokuwa yakizungumzwa.
Mtangazaji wa Kipindi cha jahazi,Mussa Hussein akijitambulisha.
Mtangazaji wa Clouds FM,B Dozen akijitambulisha
Mbwiga Mbwiguke nae kama kawa akijitambulisha kwa washiriki wa semina hiyo.
Zamarad Mketena akijitambulisha pia.

 

 Msanii wa muziki wa kizazi kipya ajulikanae kwa jina la Snura akiimba jukwaani wimbo wake unaotamba kwa sasa katika vituo vingi vya redio,uitwao  Majanga,mbele ya maelfu ya watu waliofika kwenye uwanja wa Jamuhuiri  jioni ya leo wakati wa kituo cha redio ya Clouds FM ilipokuwa ikizindua  msimu wake mpya kwa wasikilizaji wake,uzinduzi huo ulikwenda sambamba na kufanyika kwa semina ya fursa kwa Watanzania.
 Msanii mahiri wa Mashairi hapa nchini,Mrisho Mpoto akiwakuna vilivyo wakazi wa mji wa Dodoma jioni ya leo.alipowaangushia maneno kadhaa na umati kulipukw ana mayowe kila kona,ambapo Clouds FM wamezindua msimu wao mpya.
 Maelfu ya Watu wakiwa ndani ya uwanja wa jamuhuri jioni ya leo wakijumuika kwa pamoja na wana Clouds FM walipokuwa wakizindua msimu wao mpya.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya a.k.a bongofleva katika miondoko ya Hip Hop,Izzo Bizziness akikamua kwa shangwe kubwa mbele ya maelfu ya wakazi wa mji wa Dodoma waliofika ndani ya uwanja wa Jamuhuri,walipokwenda kushuhudia uzinduzi wa msimu mpya wa Clouds FM.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Madee akitumbuiza mbele ya umati mkubwa wa watu ndani ya uwanja wa jamuhuri,wakati wa kituo cha redio ya Clouds FM kilipokuwa kikizindua msimu wake mpya.
Pichani shoto ni Mkurugenzi wa vipindi na Utafiti,Ruge Mutahaba akizungumza na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye ndani ya Uwanja wa Jamuhuri jioni ya leo,wakati tamasha la uzinduzi wa msimu mpya wa Clouds FM likiendelea,Nape alifika uwanjani hapo kujionea shamrashamra mbalimbali zilizojumuisha maelfu ya watu.


Aidha msimu huo umekwenda  sambamba na kaulimbiu inayofuatia harakati za MADE IN TANZANIA,ambapo  msukumo wake ni kuwashawishi Watanzania kuanza kuzifanyia kazi fursa hizo kwa umoja wa maendeleo,huku neno TWENZETU likitumika kama neno  rasmi la mawasiliano.Kama vile haitoshi uzinduzi huo utabeba harakati  rasmi za vita dhidi ya Uharamia wa kazi za wasanii,Wabunifu na wavumbuzi
mbalimbali.Kesho kutakuwepo na matembezi ya kampeni ya kupinda uharamia wa kazi za sanii yatakayoanzia uwanja wa Jamuhuri mapema asubuhi na  kupolewa na Waziri Mkuu Mh. Pinda.

No comments:

Post a Comment