Pages

Sunday, May 12, 2013

Kifaa chanjo ya Ukimwi chagundulika

'Ugunduzi huu ni ukombozi katika kuharakisha kupatikana kwa chanjo ya ugonjwa wa Ukimwi' Dk Seif Rashid 

 

 

 Taarifa kwa Mwananchi Jumapili iliyotolewa Alhamisi wiki hii na Taasisi ya Tafiti Kukabiliana na Magonjwa ya Mzio na Kuambukiza (NIAID) ya nchini Marekani ilieleza kuwa mfumo wa kifaa hicho siyo tu utasaidia kurahisisha chanjo kukabiliana na VVU, bali hata kwa magonjwa mengine yanayosababishwa na virusi kama mafua na yale yanayosababisha uvimbe wa ini.

 

 Wanasayansi nchini Marekani wamebaini kifaa kipya kitakachoharakisha upatikanaji wa chanjo ya virusi vya Ukimwi (VVU).

Taarifa kwa Mwananchi Jumapili iliyotolewa Alhamisi wiki hii na Taasisi ya Tafiti Kukabiliana na Magonjwa ya Mzio na Kuambukiza (NIAID) ya nchini Marekani ilieleza kuwa mfumo wa kifaa hicho siyo tu utasaidia kurahisisha chanjo kukabiliana na VVU, bali hata kwa magonjwa mengine yanayosababishwa na virusi kama mafua na yale yanayosababisha uvimbe wa ini.

“Ni mfumo wa hali ya juu wenye uwezo wa haraka wa kuchambua chembechembe kinga zenye uwezo wa kuangamiza aina mbalimbali za VVU zinazopatikana duniani,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa hiyo iliyoambatanisha majina ya wanasayansi nguli wa NIAID ambao wamethibitisha kifaa hicho chenye mfumo mpya katika teknolojia ya kuchambua VVU, umeweka wazi kuwa matatizo waliyokuwa wakipata wanasayansi katika kudhibiti virusi sasa imepata ufumbuzi.

Uzuri wa kifaa hicho unaelezwa kwamba ni kuweza kuchambua na kutofautisha chembe kinga za aina mbalimbali, hata kujua idadi na uwezo wake katika kushambulia adui katika mwili wa binadamu.

“Uchambuzi wa kifaa hiki unaweza kutumika kuchunguza namna mwili wa binadamu unavyoweza kukabili maradhi mengine yanayosababishwa na virusi kama vile mafua na uvimbe wa ini,” anaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Wanasayansi nguli wa NIAID waliothibitisha uwezo wa kifaa hicho ni Mtaalamu wa Dawa na Mifumo ya Kibiolojia, ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Chanjo, Profesa Peter Kwong na Mkuu wa Idara ya Kinga, Profesa John Mascola.

Wataalamu hao wanaeleza kuwa kifaa hicho kina uwezo wa kutofautisha ni chembechembe gani za kinga zenye uwezo wa juu katika kukabili virusi vya maradhi.

Kupitia njia hiyo, inaelezwa kuwa ni rahisi kubaini chanjo yenye nguvu, hivyo kuharakisha upatikanaji wa chanjo itakayothibitishwa kukabiliana na VVU.

Kulingana na teknolojia na tafiti mbalimbali, VVU bado hajaipata tiba au chanjo madhubuti, ingawa wameweza kupata dawa zenye uwezo mkubwa wa kupunguza makali ya virusi hivyo (ARVs).

Hadi sasa tafiti mbalimbali zimeonyesha uwezekano wa kupatikana tiba na chanjo katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Kwa sasa tafiti nyingi zipo kwenye majaribio, NIAID inaeleza kuwa kupatikana kwa kifaa hicho kutaharakisha kazi ya kuchanganua uwezo wa chanjo hizo katika kukabiliana na VVU.

 

Source :Mwananchi

No comments:

Post a Comment