Pages

Tuesday, May 14, 2013

‘Mapepo’ yasababisha shule kufungwa

 

Kamanda wa Polisi Kinondoni, Charles Kenyela 

 

 Wanafunzi wa Sekondari ya Kata ya Manzese, wamedai kutokewa na hali isiyoeleweka na kusababisha wenzao 32 kuanguka na kupoteza fahamu kwa nyakati tofauti.

Tukio hilo lilianza saa 2:35 asubuhi na kudumu hadi saa 6:00 mchana. Kutokana na hali hiyo, uongozi wa shule hiyo umesitisha masomo kutwa nzima ya jana ili kuwahudumia wanafunzi hao na kuwaruhusu wengine kurudi nyumbani hadi kesho.

Mkuu wa sekondari hiyo alipofuatwa ofisini kwake kuzungumzia suala hilo, alikutwa akiombewa na Mchungaji wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), ambaye baadaye alijitambulisha kwa jina la Godfrey Alphonce maarufu kama Punda wa Yesu.

Mchungaji huyo baada ya kumaliza ibada hiyo, Mkuu wa shule alitoka akiwa ameambatana na watu wengine na alikataa kuzungumza na waandishi wa habari waliokuwapo.

“Nimechanganyikiwa naomba uniache, akili yangu haipo vizuri,” alisema mwalimu huyo na kupanda gari kisha kuondoka eneo hilo.

Kamanda wa Polisi Kinondoni, Charles Kenyela alipulizwa kuhusiana tukio hilo, alisema ofisi yake haijapata taarifa.

No comments:

Post a Comment