Pages

Sunday, May 12, 2013

BONGO MOVIE YAILAZA TASWA FC KWENYE FOOTBALL HUKU TASWA IKIWAPA KIPIGO KITAKATIFU BONGO MOVIE KWENYE NETBALL KATIKA MICHEZO YA KIRAFIKI HAPO JANA NDANI YA TCC CHANG'OMBE


Kikosi Cha Bongo Movie ambacho kimewatoa Jasho Taswa Fc
Kikosi cha Taswa FC kilichoshikishwa Kamera na timu ya bongo movie hapo jana katika bonanza la taswa na bongo movie lililofanyika katika viwanja vya TCC Chang'ombe ambapo Bongo Movie ilishinda magoli 2 kwa 0 dhidi ya Taswa fc
Mchezaji wa Taswa FC ambaye pia ndio mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari Za Michezo Juma Pinto (Mwenye Jezi ya Blue no 16) akigombania mpira dhidi ya Mchezaji wa Bongo movie katika mechi ya kirafiki iliyofanyika jana katika uwanja wa TCC Chang'ombe ambapo bongo movie iliibuka na ushindi wa Magoli 2 kwa 0
Mchezaji wa bongo movie Steve Nyerere akikimbilia mpira katika mechi ya kirafiki kati ya bongo movie na Taswa Fc iliyofanyika jana katika uwanja wa TCC Chang'ombe, bongo movie iliibuka mshindi kwa magoli 2 kwa 0 dhidi ya taswa fc.
hatari langoni mwa timu ya Taswa Fc.
Refarii wa Mechi kati ya Bongo Movie na Taswa Fc ambaye ni msanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Kiba akiwa makini kufuatilia Mchezo huo wakati mtanange ukiendelea...Refa hapo unafanya nini sasa....
Mchezaji wa bongo movie akijaribu kumtoka beki wa Taswa Fc katika mechi ya kirafiki dhidi ya Taswa Fc ambapo bongo movie ilishinda magoli 2 kwa 0.
Kipa wa taswa fc alipokuwa akijaribu kuokoa mchomo bila mafanikio na kupelekea Bongo movie kuandika goli la kwanza kwa mkwaju safi.
Wachezaji wa Bongo movie wakiwania mpira dhidi ya mchezaji wa Taswa FC jana katika mechi ya kirafiki iliyofanyika katika uwanja wa TCC Chang'ombe
Timu ya Bongo Movie ikichuana vikali katika mchezo wa mpira wa pete dhidi ya timu ya taswa queen ambapo kwenye mchezo huu bongo movie walichezea kichapo cha zaidi ya magoli 50
Mchezaji wa Bongo Movie akijaribu bahati yake ya kushinda goli dhidi ya Taswa queen katika mechi ya kirafiki iliyofanyika jana katika uwanja wa TCC Chang'ombe katika mchezo wa netball bongo movie walipokea kichapo kizito kutoka kwa Taswa queen.
Mchezaji wa Bongo Movie Jackline Wolper akijiandaa kuingia kwaajili ya kuisaidia timu yake ambayo ilipokea kichapo kizito kutoka kwa waandishi wakike wa habari za michezo taswa queen katika mchezo wa kirafiki uliofanyika jana katika uwanja wa TCC Chang'ombe Temeke.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mchezo wa netball kwa makiini wakati timu yao ikichuana na timu ya bongo movie katika mechi ya kirafiki iliyofanyika katika uwanja wa TCC Chnag'ombe ambapo Taswa queen waliibuka kwa ushindi mzito dhidi ya bongo movie.
Baadhi ya mashabiki na waigizaji wa filamu za kibongo wakifuatilia mtanange wa mpira wa miguu aka soccer wakati timu ya mpira wa miguu ya bongo ikichuana vikali na timu ya mpira wa miguu ya waandishi wa habari za michezo aka Taswa fc katika mchezo wa kirafiki uliofanyika katika uwanja wa TCC Chang'ombe hapo jana na kupelekea bongo movie kuibuka vinara kwa kuichapa taswa fc magoli 2 kwa 0.
 Baadhi ya wadau wa michezo wakifuatilia mtanange wa mpira wa miguu kati ya bongo movie na taswa fc uliofanyika jana katika viwanja vya TCC Chang'ombe na bongo movie kuibuka washindi kwa magoli 2 kwa 0
 Bloggerz wakiwa bize katika kumuzisha matukio. Kutoka Kushoto ni Othman Michuzi wa Mtaa kwa Mtaa blog, Le Mutuz William Malechela, Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa habari za Michezo TASWA Mh Juma Pinto, Muhidini Sufian  wa Sufiani Mafoto Blog, akifuatiwa na Bepari aka Lukaza the Blogger wa Lukaza Blog wakiwajibika.

No comments:

Post a Comment