Pages

Sunday, May 12, 2013

...Taharuki bomu yatanda kanisani Dar

Afande Kenyela 

 

 

Hali ya taharuki ililikumba Jiji la Dar es Salaam jana baada ya kuwapo kwa taarifa za kulipuliwa kwa bomu katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kunduchi Mtongani, Manispaa ya Kinondoni.

Taarifa hizo zilisambaa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari na kuwafanya wananchi kujiuliza nini kinalikumba taifa katika kipindi hiki.

Hali hiyo ya taharuki na mshtuko kwa wananchi inatokana na shambulio la bomu katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi la Parokia ya Olasit jijini Arusha, lililotokea Jumapili
iliyopita na kusababisha vifo vya watu watatu na majeruhi 67.

Hata hivyo, taharuki ya jana ilisababishwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni kufyatua mabomu ya machozi walipokuwa wakitekeleza operesheni ya kukamata wahalifu waliokuwa katika majengo mawili mali ya Kanisa la KKKT, Kunduchi Mtongani.

iliyopita na kusababisha vifo vya watu watatu na majeruhi 67.
Hata hivyo, taharuki ya jana ilisababishwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni kufyatua mabomu ya machozi walipokuwa wakitekeleza operesheni ya kukamata wahalifu waliokuwa katika majengo mawili mali ya Kanisa la KKKT, Kunduchi Mtongani.

Katika kutekeleza operesheni hiyo polisi hao walifunga njia zote tatu za kutoka na kuingia eneo hilo ili kuhakikisha vibaka hao hawakimbii.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Samweli Nzuna alisema kuwa baada ya kuona wanakaribia eneo hilo, polisi walifyatua juu mabomu ya machozi yaliyotoa mlio mkubwa ili kuwachanganya wahalifu waliokuwa katika majengo hayo ya kanisa wakicheza kamari na kuvuta bangi .

Alisema mara baada ya polisi hao kufyatua mabomu hayo wananchi waliokuwa karibu na eneo walianza kukimbia ovyo wakidhani jengo la kanisa limelipuliwa na vibaka hao walikimbia kuelekea katika mikoko iliyo mkabala na kanisa kabla ya polisi kufyatua tena bomu la machozi ili kuwazuia vibaka hao kukimbia zaidi.

“Wakati wa utekelezaji wa operesheni hiyo hakuna mwananchi yeyote aliyeumia ila walishtuka na wengine kudhani kuwa kanisa lilikuwa limelipuliwa kwa bomu na wahalifu, kwani awali hawakujua kama waliofanya hivyo ni polisi,”alisema Nzuna.

Naye Aloys Mwamanga, mkazi wa eneo hilo ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Wenye Viwanda na Kilimo nchini (TCCIA), alisifu operesheni hiyo akisema:

“Vibaka hawa wamekuwa wakisumbua kwa kipindi kirefu eneo hili, wameniibia hata runinga yangu hivyo naona hivi sasa amani itarejea eneo hili.”

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela alikiri tukio hilo akisema kuwa kwa sasa jeshi lake linaendesha operesheni kali ya kuwasaka wahalifu wote.

“Hivi sasa tupo katika kipindi kigumu ukilinganisha na tukio lililotokea Arusha.

 

Source: Mwananchi.

No comments:

Post a Comment