Pages

Tuesday, May 7, 2013

MBUNGE MSIGWA AWAPONZA MACHINGA ,SHERIA YACHUKUA MKONDO WAKE WANNE WAFIKISHA MAHAKAMANI KWA UCHOCHEZI

 

 

Watuhumiwa wa uchochezi dhidi ya machinga wa mbunge mchungaji Peter Msigwa akitolewa mahakamani kwa ulinzi mkali kupelekwa mahabusu baada ya kukosa dhamana leo

 

Watuhumiwa wa kesi ya uchochezi wa vurugu dhidi ya Machinga eneo la mashine tatu wakifikishwa mahakamani leo kujitu kesi ya tuhuma za uhamasishaji wa vurugu inayowakabiri ,baada ya watuhumiwa hao kudaiwa kuwahamasisha machinga kufanya vurugu jana eneo hilo la mashine tatu ambalo kisheria halitakiwi kufanya biashara

 

Ulinzi ulivyoimarishwa katika mahakama hiyo ya Mwanzo bomani leo wakati watuhumiwa hao wakifikishwa mahakakani japo hakukuwa na mtu yeyote aliyefika kwa ajili ya kuwatazama ama kuwadhamini watuhumiwa hao

Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa

...........................................................................

KAULI ya mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa ya kuwataka machinga kuvunja sheria ya mipango miji na kufanya biashara maeneo yasiyoruhusiwa imeanza kuwatokea puani machinga hao baada ya vijana wanne kufikishwa mahakamani leo na kukosa mtu wa kuwadhamini.

Vijana hao wanne wamepandishwa mahakamani leo mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya mwanzo bomani mheshimiwa Alois Masua wakikabiliwa tuhuma ya kuhamasisha mgomo kesi namba 154 ya mwaka 2013 .

Waliofikishwa mahakamani ni pamoja na Daniel Awadhi (35) mkazi wa Mkwawa , Petro Lupembe (20)mkazi wa Mwembetogwa , Baraka Muhame(32) mkazi wa Ipogolo, na Joseph Chengula (34) mkazi wa Mkwawa .

Watuhumiwa hao kwa pamoja wanashtakiwa kwa kosa la kuhamasisha mgomo kwa wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama Machinga katika eneo la Mashine tatu.

Imeelezwa mahakamani hapo kuwa watuhumiwa hao kwa pamoja walikamatwa eneo la Mashine tatu jana majira ya saa 4 asubuhi wakiwa na mabango yenye jumbe mbali mbali kwa ajili ya kuhamasisha wenzao kufanya mgomo kupinga kuzuiwa kufanyabiashara katika eneo hilo la Mashine tatu ambalo kisheria haliruhusiwi ila mbunge wao mchungaji Msigwa aliwaruhusu kulitumia.

Hivyo kutokana na sheria kutoruhusu eneo hilo kufanyabiashara watuhumiwa hao huku wakitambua kufanya hivyo ni kosa kwa mujibu wa sheria namba 74(1)(2) kifungu cha kanuni ya adhabu sura ya 16R;E 2002.

Watuhumiwa hao wamekana kosa lililowafikisha mahakamani hapo huku mtuhumiwa mmoja Petro Lupembe akiwaruka wenzake kuwa yeye kosa lake kubwa ni kutuhumiwa wizi na wananchi wenye hasira kali ndio ambao walimkamata na kumpa kichapo kiasi cha kuumizwa vibaya na wakati akikimbia kuuwawa na wananchi ndipo alipokamatwa na polisi hivyo kuiomba mahakamani hiyo kumuengua katika kesi hiyo ya machinga.

Hata hivyo mahakama hiyo haikuweza kusikiliza utetezi wa mtuhumiwa huyo hasa ukizingatia kuwa kesi hiyo ilikuwa ikifikishwa kwa ajili ya watuhumiwa kusomewa mashtaka yao .

Hakimu wa mahakama hiyo Mheshimiwa Masua alisema kuwa dhamana kwa watuhumiwa hao ipo wazi kwa kila mmoja kuwa na wadhamini wawili watakaosaini hati ya dhamana ya Tsh 500,000 kila mmoja.

Watuhumiwa hao wamekosa wadhamini na wamerudishwa mahabusu hadi Mei 20 kesi hiyo itakapotajwa tena.

Hata hivyo katika hali ya kustaajabisha ni baada ya kukosekana kwa mbunge wao mchungaji Msigwa wala msaidizi wake katika mahakama hiyo wakati chanzo cha vijana hao kukamatwa ni kutekeleza agizo la mbunge wao la kuwataka wavunje sharia.

No comments:

Post a Comment