Pages

Sunday, May 12, 2013

SCHOLES NAE ATANGAZA KUSTAAFU KUICHEZEA MAN UNITED


Wiki hii imeendelea kuwa mbaya kwa mashabiki wa Manchester United, siku chache baada ya Sir Alex Ferguson kutangaza kustaafu, leo hii kiungo wa timu hiyo Paul Scholes nae ameamua kumfuata kocha wake kwa kutundika daluga kuitumikia klabu yake pekee katika soka la kulipwa.


Gwiji huyo wa Manchester United mwanzoni alistaafu wakati wa mwisho mwa msimu wa 2010/2011, lakini akaamua kubadili maamuzi na kurejea kwenye timu mwezi January mwaka jana. 



 
 Katika taarifa yake Scholes, 38, alisema:Hatimaye ninatundika daluga zangu kabisa!
"Kucheza soka ndio ilikuwa kila kitu kwangu, na kuwa  na mafanikio kwa muda mrefu kwenye soka ndani ya Manchester United, chini ya meneja bora kabisa wa muda wote, ni heshima kubwa. 



“Timu ipo kwenye hali nzuri na itaendelea kufanikiwa chini ya uongozi wa David Moyes.” 
  Scholes amecheza zaidi ya mechi 700 akiwa na jezi ya United na kesho atakusanya medali yake ya 11 ya kombe la premier league watakapocheza dhidi ya Swansea.

No comments:

Post a Comment