MWIMBAJI wa Muziki wa Injili mwenye muonekano wa ‘mama mwenye ndoa’, Bahati Lusako Bukuku amefunguka kuwa amepata mchumba lakini tatizo linabaki kuwa mume wake wa zamani, Daniel Basila ambaye anasuasua kumpa talaka yake, Amani lina mkoba mkononi.
Akizungumza na ‘balozi’ wetu jijini Dar juzikati, staa huyo anayetamba na wimbo wake wa Dunia Haina Huruma aliweka ‘pleini’ kwamba hivi karibuni Mungu amemjalia kupata mchumba ambaye anahofia kumwanika kwa kuwa anabanwa na kifungo cha ndoa yake ya kwanza aliyofunga na Basila.
Bahati alisema kuwa kifuatacho inabidi adai talaka yake kwa nguvu zote hata ikiwezekana kufikishana polisi ili aondokane na kifungo cha ndoa hiyo na aanze mipango ya ndoa kwa kuwa hataki kumtendea Mungu dhambi.
Alisema kuwa, mara nyingi amekuwa akimkumbusha mumewe huyo wa zamani kuhusu talaka lakini amekuwa akimwambia asikonde talaka yake ipo hivyo avute subira.
Bukuku aliolewa na Daniel na kufanikiwa kupata mtoto mmoja ambaye alifariki dunia mwaka 2006 kabla staa huyo kutengana na mumewe
No comments:
Post a Comment