Mohamed Kandije (31)
Naomba
nianze kwa kutumia msemo wa wahenga kuwa Kabla hujafa hujaumbika huyu
unaye muona hapo ni Mohamed Kandije (31) mabaye ni Mkazi wa Kijiji cha
Tindinya katika Kata ya Ngapa Tarafa ya Nakapanya Wilayani Tunduru
Mkoani Ruvuma anaomba msaada wako wa hali na mali kutoka kwa watu
Binafsi na taasisi ili aweze kupata Mikono ya Bandia na kumuwezesha
walau kujitetea katika mapambano ya kimaisha.
Kama
anavyo onekana amekatwa mikono Mwezi wa 4 mwaka 2010 baada ya kupata
ajili ya kuungua na moto alipoangukia jikoni kutokana na kusumbuliwa na
ugonjwa wa Kifafa uliompata wakati huo akiwa mfanyakazi wa Kampuni ya
CONSO UNITED LTD yenye makao makuu yake katika eneo la Bandarini Mtaa
wa Kurasini Shimo la Udongo Jijini Dar es Salaam.
Baada
ya kupatwa na ajali hiyo ambayo pia ilimsababishia kupoteza viungo vya
Uzazi ambavyo pia viliondolewa pamoja na Mikono hiyo na wataalamu wa
Hospitali inayotoa huduma kwa wagonjwa wanaofanya kazi katika Mgodi wa
machimbo ya Shaba nchini Zambia.
Anasema
mkasa huo ulimpata wakati wakiwa katika eneo la Kasumbaalesi katika
mpaka wa Nchi za Congo na Zambia wakati huo akiwa msaidizi wa Shughuli
mbalimbali (UTINGO) katika Gari aina ya International mali ya kampuni
hiyo ambalo lilikuwa likiendeshwa na Dereva aliyemtaja kwa jina la
Yusuph Baisi ambaye pia toka wakati huo walipoteana na hajui aliko.
Alisema
kinacho muumiza zaidi ni Viongozi wa kampuni hiyo kumtelekeza na
kukiuka ahadi waliyo muahidi wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali
ya Mgodi huo na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili nchi Tanzania ambako
alihamishiwa kwa matibabu kuwa wangemghalamia kwa kumnunulia viungo
Bandia.
Alisema
ndoto za kupatiwa viungo hivyo zilianza kuyeyuka baada ya viongozi wa
kampuni hiyo kumkana kuwa hawakuwa wamemujiri kufanya kazi hiyo kwa
madai kuwa aliyekuwa amemtafuta ni Dereva wa gari hilo hivyo hawawezi
kuwajibika kwa lolote na hata huduma waliyo itoa kwake zilikuwa ni
fadhila la huruma yao tu.
Huku
akibubujikwa na machozi kwa uchungu Mohamedi aliendelea kueleza kuwa
kinacho muuma zaidi ni kitendo cha Viongozi hao ambao baadae pia
walianza kumkejeli kuwa akiona vipi anywe hata sumu ya panya na kujiua
iliasiendelee kuteseka na maisha hayo .
Kijana
huyo ambaye kwa sasa amepata kilema hicho cha maisha kimemtia katika
maisha ya kuwa ombaomba katika mitaa ya Mji wa Tunduru, Anasema
kuwa hali hiyo inamfadhaisha na imemfanya pia akimbiwe na Mkewe Mpendwa
Amida Mnayahe na kumuachia Mtoto wa Kiume aliye mtaja kwa jina la Rajae
Mohamed anayesoma darasa la 2 ambaye pia anashindwa kumuhudumia kwa
chakula,nguo na kumsomesha.
Kwa aliyeguswa anaombwa kumtuma mchango wake kupitia namba yake ambayo ni 0765-956-264
Na Stevie Chindiye, Tunduru
No comments:
Post a Comment