Mwaziri 15 wa baraza jipya la serikali ya Kenya walianza rasmi kazi
Alhamisi, baada ya kuapishwa na Rais Uhuru Kenyatta siku ya Jumatano.
Bunge kwa wingi mkubwa liliidhinisha Jumanne majina ya mawaziri wote 16
waloteuliwa na Rais Kenyatta.
Wachambuzi na Wakenya wengi wameeleza kuridhika na mawaziri waloteuliwa
na kuwatakia kazi njema, wakti huo huo kusifu utaratibu mpya wa
kuwachunguza kwanza bungeni kabla ya kuapishwa.
Huku serikali mpya ikichukua madaraka, hali ya wasi wasi inaendelea
katika serikali za wilaya zinazojulikana kama County, kutokana na
matatizo kadhaa ya uchukuzi, mahali ya kufanya kazi na wabunge wa
mabaraza ya County wanagoma wakidai mishahara zaidi.
Katika mjadala wa wiki wa Sauti ya Amerika "Live talk", Seneta Kipchumba
Murkomen wa County ya Ilgio Marakwet, anasema ni mapema kukosowa
utaratibu mpya wa utawala, kwani kila kitu kipya hakikosi mashaka.
Anasema inabidi kuwapati viongozi wepya nafasi kuanza kazi ndipo watu
waweze kukosowa baadae.
Mwanaharakati Afiya Rama wa Mombasa anasema utawala umeanza na
misukosuko mingi na inatia wasi wasi kwani kutokana na ukosefu wa
uwongozi thabiti kwa hivi sasa uhalifu uemezidi kote nchini, hata hivyo
inabidi kuwa watulivu na kuwapatia viongozi wepya nafasi ya kufanya
kazi.
Mbunge wa Kwamaiko County karibu na Nairobi Karungo wa Thangwa katika
"LIve Talk anasema ameweka ofisi yake kwenye soko ili kuweza kuwasiliana
na walomchagua na kumulika tatizo kubwa na watu kutokuwa tayari kwa
mfumo mpya na wawakilishi wengi hawana hata mahali ya kufanya kazi.
No comments:
Post a Comment