Pages

Wednesday, May 15, 2013

KAJALA KUIGIZA FILAMU YA MAISHA YAKE HALISI SEGEREA, APONGEZWA NA KUPONDWA.

 

 

 

News is that actress Kajala Masanja anatarajia kucheza katika filamu ambayo itaelezea maisha yake halisi ya kesi yake iliyokuwa ikimkabili. filamu hiyo itaelezea tangu mwazo wa issue hilo, mahakamani, segerea mpaka anatoka baada ya Wema Sepetu kumtolea faini ya sh. millioni 13. Kajala mwenyewe amesema ni kweli na kwasasa story na script ndiyo vinafanyiwa kazi. Hata hivyo wadau wanaweza kuwa na hamu ya kuiona filamu hiyo kama kweli itafanikiwa kuonyesha mazingira halisi ya mahakamani na segerea kama ilivyokuwa kwa mwigizaji huyo kabla ya kuwa uraiani ikichukuliwa kwamba bado ni shida sana kupata location katika taasisi za serikali hasa huko segerea ambako Kajala mwenyewe aliwahi kusema kuna mambo ya kuhuzunisha sana.

 Kwasasa inadaiwa Kajala anafanya filamu ya Princess Sasha chini ya Wema Sepetu huku tayari baadhi ya watu wakisema Kajala ana haraka sana pengine ameburuzwa na watu kuhusu kucheza story ya kesi yake kwakuwa bado mumewe yupo jela hajatoka lakini tayari yeye amepanga yake huku uraiani. Shabiki mmoja amesema " i think Kajala bado hajashauriwa vizuri kwa time hii kucheza maisha yake halisi hata miezi 2 bado kuisha". mashabiki wake wengine wamesema ni poa tu apige kazi " Kajala Nakuaminia Pamoja Sana Kazi Njema" amesema shabiki yake mmoja.



No comments:

Post a Comment