KUNDI LA KANGA MOKO MBARONI
JESHI la Polisi Mkoa wa Kinondoni, linalishikilia kundi maarufu kwa kucheza maungo yakiwa wazi ‘Kangamoko na Laki si Pesa’.
Watuhumiwa hao wamekamatwa sambamba na watu wengi wanaofanya biashara
ya kuuza miili yao, kufanya mapenzi hadharani na vitendo vya kishoga.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Kamanda wa
Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alisema kuwa kundi hilo
sambamba na watu hao walikamatwa katika maeneo ya Hoteli ya Travertine,
Ambiance Club, Kinondoni Makaburini, Coco Beach na Barabara ya Tunisia.
“Tumewakamata hao wanaofanya mchezo maarufu wa Kangamoko na Laki si
Pesa na tayari wanafikishwa mahakamani muda wowote na msako bado
unaendelea ili kudhibiti vitendo hivyo na michezo hiyo ya kangamoko au
baikoko ambayo watu wengi wameilalamikia kutokana na mtindo
wanaoutumia,” alisema.
Kundi la kangamoko limekuwa likilalamikiwa mara kwa mara kutokana na
kucheza wakionesha maungo ya miili yao wazi na kuvaa nguo nyepesi
wanazozimwagia maji.
Kukamatwa wasanii wa kundi hilo kumekuja siku chache tu tangu
walalamikiwe katika Bunge la Jamhuri ya Muungano kwamba wamekuwa
wakipotosha jamii.
No comments:
Post a Comment