Akifunguka katika mahojiano maalum wiki iliyopita na Kipindi cha
Sporah Show cha runingani alipokuwa kwenye ziara ya kimuziki nchini
humo, Diamond alizungumza ishu kibao za kimapenzi hasa juu ya msururu wa
wanawake ambao tayari ametoka nao.
ASISITIZA ANASUBIRI MTOTO
Kabla ya yote, staa huyo alisisitiza
kuwa muda si mrefu anatarajia kupata mtoto kutoka kwa mpenzi wake wa
sasa, Peniel Mungilwa ‘Penny’ akimaanisha kuwa ni mjamzito, kinyume na
msichana huyo ambaye hivi karibuni alimshangaa Diamond kueneza habari
hizo.
KWA NINI ANAPENDA KUBADILISHA WANAWAKE?
Diamond: Mimi ni binadamu
kama binadamu wengine wa kawaida. Nampenda mwanamke anayenipenda na
kuniheshimu. Ikitokea mikwaruzano huwa mimi nakaa pembeni, natafuta
sehemu nyingine. Wakati mwingine mimi ndiye huwa naachwa.
KWA NINI MSURURU NDANI YA KIPINDI CHA MIAKA MITATU?
Diamond:
Nikiwa na mtu nikiachana naye naonekana nina matatizo kwa sababu wakati
mwingine nakuwa na wanawake wenye majina. Siwezi kukaa bila uhusiano na
nakuwa wazi kwa sababu lazima itajulikana tu na kuandikwa kwenye
magazeti. Kuna kipindi nilikaa miezi sita bila kufanya kitu chochote
(mh!). Lakini nikianza (uhusiano), nikihama naonekana msumbufu.
KWA NINI MASTAA, TENA MARAFIKI?
Diamond: Huwa sitoki, nakuwa
nyumbani tu, nakaa na mama yangu (Sanura Kassim ‘Sandra’) nampikia.
Nikitoka nakwenda kwenye shoo au studio. Huko ndiko nakutana nao (mastaa
wa kike).
ALIMPATAJE JOKATE (MWEGELO)?
Diamond: Alikuwa anazindua nguo zake
(Kidoti) akaniomba nikapite nazo kwenye onesho la mavazi, nikapita nazo
jukwaani. Baada ya hapo na mimi nilimuomba nifanye naye video ya wimbo
wangu (Mawazo), ndiyo ikatokea kama hivyo.
NINI KILIMVUTIA KWA PENNY?
Diamond: Kwanza mimi nilimjua Penny
kabla ya Wema (Sepetu), alikuwa mshikaji wangu. Ni mwanamke mzuri, wa
kileo, ana akili adabu na heshima. Anampenda mama yangu na familia yangu
‘coz’ na mimi nampenda mama yangu (sifa ambazo kwa mujibu wake Wema
alizikosa).
KWA NINI ALIMREKODI WEMA?
Diamond: Kila binadamu anajiona yupo
sawa na anaonewa. Sipendi kuongea, nitazungumza vibaya. Mapenzi
yanaumiza na mimi naumia pia lakini watu wanadhani mimi ndiye muumizaji.
Unamwambia mtu kwa nini una mwanaume mwingine.
Anakuzuga sijui ni
pedeshee anampa pesa. Mara unamwona na mwanaume mwingine. Mimi siyo
maskini lakini sasa mara unamwona na brazameni mwingine ‘then’ washkaji
wanakwambia. Wewe unajifanya kuziba masikio mara unasikia ana mwanaume
mwingine. Lakini ikafika wakati nikajikuta naumia sana kwenye mapenzi.
Kama ukisikiliza ule wimbo wa Kesho ni kweli kabisa. Mimi nikakaa pembeni hadi nilipompata huyu wa sasa (Penny).
Nakumbuka (Wema) alinipigia simu akadai mimi ndiye nasema anataka turudiane. Nilikuwa kwenye gari, nikamuuliza anataka nini?
Wakati
huo nilishafika nyumbani kwa baby wangu. Nikamwonesha ona sasa, anasema
mimi ndiyo nataka nirudiane naye, anatangazia watu hadi saluni kuwa
nataka kurudiana naye na kujidai kwenye vyombo vya habari kuwa
ananipenda. Kumbe ana wengine (ving’asti) kama ishirini anawahonga
(mistari ya wimbo wake wa Nataka Kulewa).
Nilimpa baby wangu akamwambia kistaarabu tuache tulale. Sasa kuna mtu wetu wa karibu ndiye aliyehusika kusambaza ile sauti.
SEMA UKWELI, ULILALA NA UWOYA?
Diamond: (kicheko) Ningeanzia wapi?
Unajua mimi ni simba kwa hiyo nikionekana na swala inajulikana lazima
nimle hata kama tumeenda sehemu tu kuzungumza ishu za kazi.
KWA NINI WANAWAKE AU ENZI ZILE HAKUWA NA ‘CHANSI’ SASA AMEPATA?
Diamond:
Ukimuelimisha mwanamke mmoja umeelimisha ulimwengu mzima. Nawapenda
sana, wanajaa tele kwenye shoo zangu. Kilichotokea kwa Wema ilibidi tu
sikuwa na jinsi.
ANATAKA MWANAMKE WA AINA GANI?
Diamond: Ukimuuliza mwanamke
aliyewahi kuwa na mimi atakwambia najua mapenzi, najua kupetipeti, najua
kubembeleza, najua kujifanya mjinga. Narudia tena, awe mzuri, wa kileo,
mwenye akili, anayejiheshimu, ampende mama yangu kama mimi
ninavyompenda mama yangu.
KWA NINI KIWEMBE?
Uchunguzi
uliofanywa ulibaini kuwa chanzo cha staa huyo aliyetokea
Tandale, Dar kuitwa kiwembe ni kutokana na tabia yake ya kubadilisha
wanawake kama nguo.
Baadhi ya aliowahi kuripotiwa akidaiwa kutoka nao
ni Rehema Fabian (Miss Kiswahili 2009), Jacqueline Wolper (msanii wa
filamu), Upendo Moshi ‘Pendo’ (Mshiriki wa Maisha Plus) na Natasha
(Video Queen wa Bongo Fleva).
Wengine ni Wema (mwigizaji), Jokate
(mwigizaji), Aunt Ezekiel (mwigizaji), Najma (msanii wa Bongo Fleva),
Penny (mtangazaji DTV), Irene Uwoya (mwigizaji) na wengineo.
No comments:
Post a Comment