MAMBO YANAZIDI KUNOGA .... DULLY SYKES KUPAMBA USIKU WA REDDS MISS MOSHI 2013 AVENTURE
|
Dully
Sykes
|
MSANII wa muziki wa
kizazi kipya wa Bongo Fleva, Dully Sykes "mista Misifa" anatarajia kupanda jukwaani
kutumbuiza katika usiku wa Ulimbwende, usiku wa Redds Miss Moshi 2013
yatakayofanyika May 18, katika ukumbi wa Aventure, Mjini Moshi.
Akizungumza mratibu wa
mashindano hayo, Mkurugenzi wa kampuni ya New Vision plan inayohusika na kazi za
kuandaa mashindano ya ulimbwende, Moses Komba alisema kuwa jumla ya warembo19
watachuana kumsaka malkia wa Moshi wakisindikizwa na Prince Dully
Sykes.
Moses alisema tayari maandalizi yameshaanza na
mchujo wa kwanza umeshafanyika ambapo warembo wote wameshaingia kambini kujifua
na kuongeza kwamba mashindano ya mwaka ambayo ni ya pili tangu yaanzishwe
yatakuwa ni ya aina yake.
“Maandalizi yameshaanza, warembo wote wapo kambini
hapa katika ukumbi wa Aventure, kutoa burudani atakuwepo mtu mzima Prince Dully
Sykes, kila kitu kinakwenda sawa na tunategemea kushuhudia kitu tofauti na yale
ya mwaka jana,” alisema Komba.
Kuhusu swala la udhamini alisema bado hilo ni
tatizo huku wadhamini wakuu Redds na kampuni ya panone kwa kujitolea kudhamini
mashindano hayo. Akitangaza viingilio katika mashindano ya mwaka huu, Komba
alisema kuwa kwa viti vya dhahabu viingilio vitakuwa sh. 50,000, viti vya V.I.P
vitakuwa ni sh. 30,000 na viingilio vya kawaida ni sh. 15,000.
Kwa upande baadhi ya washiriki wa Redds Miss Moshi,
wakizungumza na Gazeti hili katika kambi ya mazoezi, Jacky Mushi, Winlady Mushi,
Aichi Edwin na Rayness White walisema kuwa wabnatarajia kutumia uzoefu
watakaoupata kutoka katika mashindano hayo kulitumikia jamii hasa wale waishio
katika mazingira magumu.
Mashindano ya Redds Miss Moshi 2013 yatakayofanyika
katika ukumbi wa Aventure, yanadhaminiwa na Redds, Panone na Baba G na Zoom Net
Printers ambapo kwa upande wa burudani alisema atakuwepo msanii mkongwe wa
kizazi kipya Dully Sykes akisindikizwa na wasanii wengine kutoka
Moshi.
No comments:
Post a Comment