Ndugu Mtangazaji fetty
YAH; MAJIBU YA MASWALI YA WADAU KUHUSU BEN POL LOVE CD AMBAYO NILIAHIDI KUITOA MWEZI ULIOPITA.
Husika
na kichwa cha barua hapo juu, Mimi ni mwanamuziki wa Kizazi
kipya ninayefanya shughuli zangu za Muziki hapa hapa jijini Dar ES
salaam
Nilianza kufanya shughuli za Kimuziki mnamo mwaka 2010 na
kufanikiwa kutoa vibao Kama Nikikupata, Number 1 fan, Samboira
nakadhalika, na hiyo ilinipelekea kujizolea mashabiki lukuki, na
ninamshukuru Mungu maana pia nilifanikiwa na kutoa Albamu ya kwanza
(Maboma) iliyotoka mwezi Februari mwaka 2011 na kusheheni vibao
vinavyopendwa na kunifanya kupata mialiko mbalimbali na kupata
japo Riziki.
Mnamo mwezi Aprili mwaka 2013 nilitangaza kuwa ningetoa "CD"
yangu ya Pili niliyoipa jina la "Ben Pol Love CD" ambayo ingesheheni
nyimbo 18, na tayari maandalizi yalikuwa katika hatua za mwisho
kukamilika.
Ninasikitika na ninaomba radhi kwamba nilishindwa kufanya hivyo
kwa wakati, na hiyo ilitokana na shughuli za upigaji picha wa video ya
wimbo wangu mpya "Jikubali" ambayo niliifanyia Jijini Arusha na
kunigharimu muda mwingi na gharama kuliko ilivyotarajiwa hapo
mwanzoni, hivyo kunilazimu kusitisha shughuli zote kwa muda ili kufanya
jambo moja kwa nafasi zaidi.
Napenda nikuahidi Mtanzania mwenzangu pia Shabiki na Mdau wa
muziki kwamba "Ben Pol Love CD" iko pale pale na itatoka, tarehe na
mwezi wa kuitoa nitaitangaza hivi karibuni mara tu baada ya kupata Video
ya Jikubali na kui-schedule kwamba nayo inatoka lini.
Mwisho napenda kukushukuru kwa kusikiliza barua yangu, na kwa mchango wako katika muziki wangu.
Kwa sasa kuelekea kwenye kilele cha Utoaji wa tuzo za Kilimanjaro
Tanzania Music Awards kwa mwaka 2013, unaweza kuniwezesha kushinda
Tuzo katika vipengele vifuatavyo;
Wimbo bora wa Mwaka "Pete" tuma SMS "AA5" kwenda 15345
Wimbo bora wa RnB -Maneno Maneno SMS "BU3" kwenda 15345
Wimbo bora wa RnB -Pete SMS "BU4" kwenda 15345
Msanii bora wa kiume (Kiujumla) SMS "AF2" kwenda 15345
Msanii bora wa kiume (Bongo Flavour) SMS "AB1" kwenda 15345
Mtunzi bora (Bongo Flavour) SMS "AU3" kwenda 15345
Natanguliza shukrani zangu za dhati,
Wako katika ujenzi wa Taifa,
BEN POL
Benard Paulo
Dar ES salaam, Tanzania
No comments:
Post a Comment