Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa
Siku
mbili baada ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman
Kinana, kumtaka Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa
kufuta kashfa dhidi yake, mbunge huyo ameibuka na kusema kamwe hatafuta
kauli hiyo aliwahi kuitoa bungeni na katika mikutano ya hadhara.
Alisema ana ushahidi wa kutosha kuthibitisha tuhuma dhidi ya mtendaji huyo mkuu wa CCM.
Mchungaji Msigwa aliwahakikishia wapigakura wake kuwa hana hofu juu ya msimamo huo na kwamba yuko makini kwa kila anachokifanya.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika
katika Viwanja vya Mashine tatu katika Manispaa ya Iringa juzi, mbunge
huyo alisisitiza kuwa tuhuma hizo ni za kweli.
Alisema tuhuma hizo alikuwa amezitoa bungeni lakini pia katika mikutano mbalimbali ya hadhara na kwamba ana ushahidi nao.
Alisema siku 21 zilizotolewa na Kinana kupitia kwa
wakili wake Erick Ng’maryo kumtaka afute kauli hizo, ni chache na
kwamba yeye yupo tayari kwenda mahakamani wakati wowote kuanzia sasa.
“Nilipotoa hotuba yangu bungeni nilimtuhumu Katibu
Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kuwa anahusika na matukio ya ujangili ya
uwindaji wa wanyamapori wakiwemo tembo hapa nchini. Sasa katibu huyo
amenipa siku 21 nifute kauli yangu na nimwombe radhi, mimi ninasema
siombi radhi nasubiri wito kwa kwenda mahakamani,”alisema Msigwa.
“Kinachonisikitisha zaidi wametoa taarifa hiyo
kama maelezo makubwa ya kujisafisha kwenye gazeti huku mimi wala ofisi
yangu ikiwa haijapatiwa barua yoyote,”alisema.Alisema hadi kufikia jana,
alikuwa hajapata barua rasmi kutoka kwa wakili wa Kinana kumtaka aufite
tuhuma hizo.
No comments:
Post a Comment