MLINZI wa baa ya Darajani Stop Over iliyo kando kando ya barabara kuu ya Morogoro=Dar es salaam jirani na daraja la Mzambarauni mkoani hapa Bw Mika Athumani amechinjwa na majambazi usiku wa kuamkia leo.
Habari zilizoptaikana eneo la tukio zilidai kwamba majambao hao baada ya kuvamia baa hiyo iliyojitenga usiku wa manane na kumvamia mlinzi huyo na kumchinka kama kuku na baadae kuvunja baa hiyo na kuimba vitu mbali mbali.
Akihojiwa na Mtandao huu mmiliki wa baa hiyo Bw Salvatory Mushi alidai kwamba majambao hao walimvamia mlinzi wake na kumchionja bna baadae walivunja Counter ya baa hiyo pamoja na duka ililipojirani na baa hiyo na kuiba vitu mbali mbali.
Alipoulizwa kwamba kuna taarifa zinadai kwamba mlinzi huyo alikutwa akiwa amelala Bw Mushi alisema" inawezekana lakini hakuna mtu mwenye uhakika na jambo hilo kwani sote hatukuwepo,wakti tukio hilo linatokea"alisema Bw Mushi ambaye anadai bado hajafahami dhamani ya vitu vilivyoibikiwa na majambazi hayo.
Mwili wa marehemu ukiwa ndani ya gari, la polisi kufuatia mwili huo kutenganiswa vibande viwili mtandao huu umesita kuweka picha hiyo
Baadhi ya watu waliokuwepo eneo hilo la tukio walidai kwamba mlinzi huyo alikuwa amelala hivyo majambazi hayo yalimvamia na kumpora siraha zake na kishi kumchinja shingoni," siumeona alikuwa amelala jirani na baiskeli yake ndio maana ameshindwa kupamabna nao hasa ukizingatia baa hii imejitenga iko peke yake hapa jirani na mto wa Morogoro"alisema Bw Maneo Mashani.
Mtandao huu ulishuhudia mtoto wa marehemu pamoja na mjukuu wa marehemu wakiangua vilio eneo la tuko baada ya kuuona mwili wa mazazi wao aliyeuwawa kikatili baadae wote wawili walipanda gari la polisi na kuondoka nao.
No comments:
Post a Comment