JUKWAA
la Wahariri Tanzania (TEF) limemsimamisha uanachama kwa muda
usiojulikana, Mhariri wa Mtanzania Jumatano, Charles Mulinda, kwa sababu
za kukiuka maadili ya uandishi wa habari, li,eandika gazeti la Tanzania
Daima la leo
Taarifa
iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu wa Jukwaa hilo, Neville
Meena(Pichani), alisema TEF imechukua uamuzi huo baada ya kupokea na
kujadili kwa kina taarifa ya kamati ndogo ya wahariri watatu ambayo
iliongozwa na Mhariri wa Nipashe, Jesse Kwayu, kwa ajili ya kuchunguza
habari iliyochapishwa na gazeti la Mtanzania, Jumatano Aprili 17, mwaka
huu ikiwa na kichwa kisemacho ‘Mtandao Hatari’.
Katika
habari hiyo, Meena alidai kuwa iliwataja wahariri wawili, Ansbert
Ngurumo wa Tanzania Daima na Deodatus Balile wa Jamhuri kuwa ni
washirika wa Joseph Ludovick, mshitakiwa katika kesi ambayo ilikuwa
ikihusishwa na ugaidi (kabla ya kubadilishwa na mahakama) lakini
ikiwahusisha kwa namna moja au nyingine na tukio la kuumizwa kwa
Mwenyekiti wa TEF, Absalom Kibanda.
“Yalikuwa
ni maoni ya wahariri wengi katika mkutano wa Aprili 18, 2013, kwamba
habari hiyo ilikuwa na upungufu mkubwa kitaaluma, hivyo kuamua
kuchunguza habari hiyo na kubaini iwapo kulikuwa na ukiukwaji wa maadili
na misingi ya kitaaluma ya habari.
“Pamoja
na mambo mengine ilipaswa kuchunguza mazingira ya kuchapishwa kwa
habari hiyo na kama kulikuwa na msukumo wowote nyuma ya kuandikwa kisha
kuchapishwa kwakwe,” alisema.
Meena
alisema kamati hiyo ilipaswa kuchunguza ushahidi wa tuhuma zilizotolewa
dhidi ya Deodatus Balile na Ansbert Ngurumo (kama Mullinda)
alivyokiambia kikao cha Aprili 18 kwamba alikuwa na ushahidi wa yale
aliyoyaandika.
Aliongeza
kuwa TEF ilibaini kulikuwa na ukiukwaji wa maadili ya kitaaluma katika
mchakato mzima uliowezesha kuandikwa na kuchapwa kwa habari husika na
kwamba habari hiyo haikuwa na sifa wala vigezo vya kihabari.
Hata
hivyo, Meena alisema Mulinda alipotakiwa kutoa ushahidi wa tuhuma dhidi
ya wahariri aliowataja, alishindwa kuthibitisha usahihi wa taarifa
hiyo.
Kwa
kuzingatia matokeo hayo TEF inaushauri uongozi wa New Habari (2006) Ltd
na vyumba vingine vya habari kuboresha mfumo wake wa usimamizi wa
uhariri ili kuziba mianya kwa habari tata kama hiyo ya ‘Mtandao Hatari’
kupenya na kuwaumiza baadhi ya watu bila kuwapo kwa uthibitisho wa
tuhuma husika.
TEF
inaendelea kuchukua hatua nyingine za ndani kuimarisha usimamizi wa
nidhamu na maadili kwa wahariri, na itaendelea kuchukua hatua dhidi ya
ukiukwaji wowote ule wa kitaaluma utakaofanywa katika vyombo vya habari.
No comments:
Post a Comment