Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Charles Kenyela.
USTADHI aliyetajwa kwa jina moja la
Ahmad (38) anayefundisha Chuo cha Tawfiq kilichopo Kinondoni B, Dar
ambaye pia ni mfanyabiashara, anashikiliwa na polisi kwa madai ya
kuwalawiti watoto watatu ambao ni wanafunzi wa Shule ya Msingi Msisiri.
Watoto hao (majina yanahifadhiwa kwa
sababu za kimaadili) wawili kati yao ni wanafunzi wa darasa la nne na
mmoja ni wa darasa la tano katika shule hiyo.
WAZAZI SOMENI KWA MAKINI HAPA
Wakisimulia kisa hicho, watoto hao
walisema, Ustadh Ahmad ambaye ni Mpemba anayemiliki duka lililopo jirani
na shule wanayosoma watoto hao, amekuwa na tabia ya kuwarubuni kwa
juisi na keki.
Katika maelezo yao kwa mwandishi wa
habari hizi, mmoja wa watoto hao alisema: “Kama mimi nilikuwa nikipita
kwenda shule ananiita ndani ya duka kisha anafunga na kunipa juisi na
keki.
“Mara ya pili, akanipa tena juisi halafu akanipaka sijui ni mafuta gani yale halafu akanifunga kamba mikononi na miguuni.”
Anaeleza kuwa baada ya hapo,
alimfunga kitambaa mdomoni ili asiweze kupiga kelele kisha akamwingilia
bila huruma na kwamba alimtishia kuwa akisema atamuua, maelezo ambayo
yaliungwa mkono na watoto wote.
MWALIMU MKUU ANASEMAJE?
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi
Msisiri, Suzan Orege alipoulizwa kuhusu tukio hilo alisema: “Hawa watoto
walianza tabia ya utoro, ndiyo tukaamua kuwaambia waje na wazazi wao.
Cha kushangaza, wazazi wakasema watoto wao huondoka kila siku nyumbani
kwenda shuleni.
“Tukawapa adhabu kali na kuwauliza
wanapokwenda ndipo walipomtaja huyo mwanaume. Sisi kama shule tukaamua
kuripoti suala hilo polisi na tunashukuru walifika na kumchukua. Sasa
tunaacha sheria ifanye kazi yake.”
Kesi ya Ahmad ipo Kituo cha Polisi
cha Oysterbay jijini Dar na imepewa jalada namba OB/RB/8252/2013,
OB/RB/8253 na OB/RB/8253, uchunguzi unaendelea na watoto hao walipelekwa
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.
No comments:
Post a Comment