Hatimaye
fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania mwaka huu,zinafanyika mkoani
Tanga siku ya Jumapili Tarehe 19-5-2013katika uwanja wa CCM Mkwakwani
Tanga. Fainali hizo za tano za Taifa za mashindano ya Miss Utalii Tanzania
tangu kuanzishwa kwake mwaka 2005, zitajumuisha jumla ya warembo 30
kutoka mikoa yote ya Tanzania, na vyuo vikuu watapanda jukwaani kuwania
taji la Taifa la Miss Utalii Tanzania 2012/13.
Zawadi
kwa mshindi wa kwanza ni mkataba wenye thamani ya sh.90,
000,000/=,ambao unajumuisha skolashipu ya kusoma kozi ya Diploma katika
chuo cha Dar es Salaam City Collage, safari za kushiriki mashindano ya
Dunia,ziara za Tanzania Great Safari and Tour 2013, kugharamiwa usafiri
wakati wa shughuli za kutekeleza majukumu yake ya ushindi,na shilingi
5,000,000/= baada ya kutumikia taji lake wakati wa kukabidhi kwa mshindi
wa msimu ujao.
Aidha
mshindi wa pili hadi wa tano, kila mmoja kila mmoja atajipatia mkataba
wenye thamani ya shilingi 58,000,000/=, ambao pia unajumuisha skolaship
za kusoma chuo cha Dar Es Salaam City Collage na safari za kushiriki
mashindano ya kimataifa nay a dunia, pia ushiriki wa safari za Tanzania
Greet Safari and Tour 2013 na kugharamiwa usafiri wakati wa utekelezaji
wa majukumu yao ya ushindi. Washiriki walio bakia watajipatia tuzo
mbalimbali za heshima, za utalii, utamaduni, jamii, uchumi, mitindo,
,wanyama pori,misitu,mazingira,utalii wa ndani,utalii wa
kitamaduni,jinsia,utalii wa michezo,utalii wa mikutano,elimu ya
jamii,afya ya jamii, urembo na maliasili.
Mashindano
ya Dunia ambayo washindi hao watashiriki ni Miss Tourism World 2013,
Miss Tourism United Nation 2013, Miss Tourism University World 2013,
Miss Heritage World 2013, Miss United Nation 2013,Miss Freedom Of The
World 2013,na Miss Globe International 2013.
Burudani
katika fainali za mwaka huu ,zitakazo fanyika kitaifa mkoani tanga
jumapili tarehe 19-5-2013, ni pamoja na Bendi ya Msondo Ngoma, Mwana
mziki wa kimataifa Che Mundu Gwao, Ngoma za asili na vichekesho kutoka
kundi la Majuto Arts Group linalo ongozwa na mwigizaji mahili na mkongwe
Mzee Majuto,sarakasi na muziki wa kizazi kipya yani bongo
fleva.Maandalizi yamekamilika, na hali ya kambi ni shwari huku washiriki
wote wakiwa katika hali ya kujiamini, kila mmoja akijigamba kupeleka
jaji mkoani kwake mwaka huu.
Katika
shindano la mwaka huu, katika ukumbi wa CCM Mkwakwani, wabunge
,madiwani,wakuu wa wilaya,na viongozi wa vyama na serikali wamealikwa
kuhudhuria. Mkuu wa mkoa wa Tanga Mheshimiwa Chiku Galawa atakuwa mgeni
rasmi katika fainaali hizo za kihistoria kufanyika mkoani Tanga.
Tumepeleka
fainali za jumapili katika uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga, ili kutoa
fulsa kwa wakazi wa kada zote kushudia fainali hizo, kwani shindano hili
ni kwa ajili ya watanzania wote
bila kujali utofauti wao wa vipato wala umri,ndo mana viingilio ni vya
beii ya chini sana, ambapo shindano litaanza mchana wa saa 7 hadi usiku
wa manane. Viingilio watoto itakuwa 2000/=, wakubwa mzunguko itakuwa
shilingi 5,000/=, viti maalum shilingi 20,000/= na viti vya kawaida ni
shilingi 10,000/=.
No comments:
Post a Comment