
|
Mhe. Zitto Kabwe
|
Baada ya malalamiko ya muda mrefu sana kuhusu wanamuziki kutofaidika na
biashara ya miito ya simu (ring back tones - #RBT), hatimaye Waziri wa
Viwanda na Biashara Dkt. Abdallah Kigoda ameagiza #COSOTA kufanya
marekebisho ya kanuni ili kuweka kiwango cha mrabaha Kwa wasanii kutoka
pato ghafi la biashara hiyo Kwa kampuni za simu.
Vile vile kanuni namba 3 ya Kanuni za Sheria ya Hakimiliki, Sheria namba
7 ya mwaka 1999 itaanza kutumika rasmi na hivyo wasanii kulipwa mrabaha
kutokana na nyimbo zao kupigwa kwenye vituo vya redio na televisheni.
Agizo hili la Waziri Kigoda linavunjilia mbali mfumo wa kinyonyaji
uliokuwa unafanywa na kampuni za simu Kwa kuuza kazi za wasanii bila
mikataba na kujiamulia wenyewe Kiwango Cha malipo. Uamuzi huu Ni
ukombozi Kwa wasanii wetu.
Watumie mapato haya makubwa watakayopata kuwekeza kwenye kuboresha kazi
zao na kuwa na uwezo wa kuingia mikataba bora zaidi Kwa kuajiri
wanasheria mahiri. Shime wasanii wetu, kazi kwenu!
No comments:
Post a Comment