WEMA SEPETU NA KAKA YAKE DIAMOND KUWA WAWAKILISHI WA BIG BROTHER AFRICA 2013 !
Wema Sepetu
Habari za chini chini ni kuwa actress Wema Sepetu ambaye pia ni Miss
Tanzania mwaka 2006 yeye na Romeo Rommy Jones ambaye ni ndugu yake
Diamond Platinumz ndiyo watakuwa wawakilishi wa Tanzania katika shindano
maarufu barani Afrika, Big Brother Africa 2013(BBA) ambalo mwaka huu
linaitwa " BBA The chase".
Chanzo kimoja kimeitonya Swahiliworldplanet
huku kikikataa kutajwa jina lake. Kimesema kuwa yeye ameambiwa na rafiki
yake ambaye anafanya kazi DSTV lakini hakumhakikishia kwa asilimia zote
huku akisita kuweka wazi na kubaki kucheka tu alipomuuliza kama Wema na
Romeo ndiyo watakuwa wawakilishi.
Ukiachana na chanzo hicho mtu
mwingine jana aliambia Swahiliworldplanet kuwa alisikia mfanyakazi mmoja
wa DSTV pia akitaja jina la Wema katika mazungumzo yaliyokuwa
yanahusiana na shindano hilo lakini alishindwa kuyafuatilia kwakuwa
alikuwa anaondoka na gari na kuwaacha waliokuwa na mazungumzo hayo. "t
iz likly wema ndo ataend kula upepo BBA, i hed employee dstv aki-mention
jina lake ktk talk related to bba bt nliondka na gari bila info ya
ukwel ". kilisema chanzo hicho.
Wakati form za shindano hilo zilipotoka zilisambaa habari kuwa Wema
alichukua form kwa ajili ya kujaribu bahati yake katika shindano hilo
lakini meneja wake Martin Kadinda alisema si kweli.
Jana katika
instagram Wema aliweka picha akiwa na Romeo ambaye wiki iliyopita habari
zilianza kusambaa kuwa yeye ndiye mwakilishi wa BBA mwaka huu lakini
mwenyewe alipoulizwa na gazeti moja alibaki kucheka tu huku ikidaiwa
kama alikuwa akificha kitu chenye ukweli ndani yake.
Inadaiwa Wema na
Romeo wameanza kuwa karibu kwa ajili ya issue hiyo na chanzo hicho
kikidai kuwa hata safari ya Wema kwenda Dodoma akijitia kudai maslahi ya
wasanii ni moja ya mipango yake ili apate kura za watanzania akiwa
mjengoni huko S. Afrika.
Hata hivyo inadaiwa DSTV hawapo tayari kuweka
jina la mwakilishi mpaka siku ya ufunguzi rasmi wa shindano hilo mwezi
huu kuku ikidaiwa kuwa baadhi ya nchi zitatoa mwakilishi zaidi ya mmoja
kwakuwa wanatakiwa wawakilishi 28 huku nchi zinazoshiriki zikiwa 14 au
kila nchi kutoa wawakilishi wawili.
Je hii ni kweli au uvumi tu? lets
wait n see
No comments:
Post a Comment