Kipa
wa Simba, Juma Kaseja, akitaabika chini baada ya kushindwa kuuokoa
mpira wa kichwa uliopigwa na Didier Kavumbagu, katika dakika ya 5 na
kuandika bao la kuongoza katika kipindi cha kwanza. Simba nao walipata
penati dakika chache baadaye baada ya Canavaro kumuangusha Ngassa katika
eneo la hatari na petati ikapigwa na Mussa Mude aliyempelekea kipa
katika engo ya kushoto kwake na kuokolewa na kipa huyo.
Mshambuliaji
wa Yanga, Simon Msuva, akichuana na beki wa Simba, Shomari Kapombe, na
mpira huo ulitoka na kuwa kona iliyozaa bao. Sasa mpira ni kipindi cha
pili, kaa na ukurasa huu utakaokuletea full matukio ya mechi hii ya
Watani wa jadi.
No comments:
Post a Comment