DEMU AMFANYIA TIMBWILI HEMED
STAA
mwenye swaga za kupitiliza Bongo, Hemed Suleiman ‘PHD’ amepatwa na
masaibu ya kutaka kushushiwa kipondo hevi na demu ambaye jina lake
halikupatikana mara moja baada ya kumpulizia pafyumu bila ridhaa yake.
Tukio
hilo liloloonekana kumkosesha amani PHD, liliibuka Jumapili iliyopita
ndani ya Ukumbi wa Bilicanas, Posta, jijini Dar wakati staa huyo
alipokuwa akizindua singo yake mpya inayofahamika kwa jina la Rest of My
Life.
Chanzo
makini kilichoomba hifadhi ya jina, kilimtonya paparazi wetu kuwa
wakati staa huyo akipafomu jukwaani alishika pafyumu kama swaga za
kunogesha shoo huku akiwapulizia baadhi ya mashabiki wake, haswa
warembo.
Aliwapulizia
pafyumu baadhi ya warembo akiwa jukwaani lakini kumbe kitendo kile
hakikumpendeza mdada mmoja hivi aliyeonekana kama ni shombeshombe.
“Sasa
akaona isiwe tabu, akasubiri aliposhuka jukwaani, akamfuata nyuma ya
jukwaa (back stage) na kuanza kumshika shati huku akihoji kwa nini
alimpulizia pafyumu hiyo bila ridhaa yake,” kilisema chanzo hicho.
Wakati
mwanadada huyo akiwa amemtaiti PHD, baadhi ya watu waliokuwa karibu
waliingilia kati na kumsihi dada huyo apunguze munkari, zoezi ambalo
lilichukua takriban robo saa.
Hemed alifanikiwa kuchomoka kwenye himaya ya mlimbwende huyo na kumwacha akiendelea kumchimba biti.
Juhudi
za kumpata Hemed juzi Jumanne ili aeleze kwa undani kilichompata
hazikuzaa matunda baada ya simu yake ya mkononi kutopatikana hewani.
chanzo:globalpublishers.
No comments:
Post a Comment