AHADI
nyingi zilizotolewa na Rais Jakaya Kikwete wakati wa uchaguzi mkuu 2010
zimeanza kuwatia hofu ya kushindwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015
wabunge wa CCM.
Wabunge hao wa CCM walisema endapo ahadi hizo hazitatekelezeka chama hicho kitarajie kuanguka katika uchaguzi mkuu ujao.
Wakichangia
hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Uchukuzi kwa
mwaka 2013/2014 bungeni mjini hapa, wabunge wengi wa CCM walimtaka Dk.
Harrison Mwakyembe wakimtaka ahakikishe ujenzi wa reli, viwanja vya
ndege, meli na bandari vinakamilika kabla ya 2015.
Mbunge wa
Nzega, Dk. Khamis Kigwangala Mwakyembe kwa kushirikiana na waziri
mwenzake wa ujenzi, Dk. John Magufuli kuhakikisha wanaufungua Mkoa wa
Tabora kwa usafiri wa reli, anga na barabara.
“Tabora
imechagua wabunge wote wa CCM 2010, lakini leo haifikiki kwa usafiri
wowote iwe reli, ndege wala barabara. Na hatua hiyo imewafanya wapinzani
hasa CHADEMA na CUF kutuchonganisha kwa wananchi kuwa umasikini wao
umetokana na kuichagua CCM.
“Sasa
Mwakyembe kwa kushirikiana na Magufuli hakikisheni mnaifungua Tabora kwa
kutekeleza ahadi za rais, vinginevyo uchaguzi ujao 2015 CCM itakuwa
janga,” alisema.
Alisema kuwa
Serikali ya CCM inapaswa kulifufua Shirika la Ndege (ATC) kwa kukopa
ndege kama wanavyofanya mataifa mengine akiitolea mfano Rwanda
iliyonunua ndege mpya kwa utaratibu huo.
“Waziri
Mwakyembe naamini una akili timamu, una uwezo wa kufanya hayo. Na sisi
ukiyafanya hayo hata mwaka 2015 tunaweza kukufikiria kwenye ile nafasi
(akimaanisha urais),” alisema.
Mbunge wa
Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani alimtaka Mwakyembe alieleze Bunge ni
kwanini miradi yote wizara hiyo aliyoahidi Rais Kikwete haitengewi
fedha.
Alisema kuwa
wananchi wanahoji kiwanja cha ndege Tanga mjini, upanuzi wa bandari ya
Tanga na ujenzi wa bandari mpya ya Korogwe, huku akioneshwa kusikitishwa
na uamuzi wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo wakati ile ya Tanga ikiwa
haijatekelezwa.
“Waziri
aniambie kiwanja cha ndege Tanga kiko wapi kwenye bajeti yake,
tuliahidiwa reli kufufuliwa na kwenda hadi Musoma. Viwanja vya ndege
Same, Arusha na Moshi tulivyoambiwa vimetengewa fedha mwaka jana vipi,”
alisema.
Ngonyani,
maarufu kama Majimarefu aliongeza kuwa waliokuwa wafanyakazi wa reli
Tanga waliahidiwa kulipwa madai yao lakini hadi sasa bado, na hivyo
kuonya kuwa bila mambo hayo kufanyika hali itakuwa ngumu kwa CCM 2015
licha ya majimbo yote kukaliwa na chama hicho.
Hata hivyo,
wakati CCM wakihofia kuangushwa 2015, wabunge wa upinzani wamekuwa
wakishangilia hatua ya serikali ya chama hicho kushindwa kutekeleza
ahadi zake wakisema kimechoka kutawala.
Akichangia
hotuba hiyo, Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga, Amina Mwidau (CUF),
alisema kuwa serikali ya CCM ilichowafanyia wananchi wa mkoa huo kwa
kutowajengea bandari waliyoahidiwa na badala yake bandari hiyo
kuhamishiwa Mbegani Bagamoyo ni sawa na kujipa talaka.
“Hii ndiyo
talaka yenu CCM, majibu yake mtayaona 2015 kwenye uchaguzi mkuu. Wenzetu
Kenya wamekopa wakajenga bandari ya kisasa Lamu, wanayo Mombasa na sasa
wana mpango wa kujenga nyingine Shimoni, sisi Tanga tutakuwa wapi kama
ahadi yetu imepelekwa Bayamoyo?” alihoji.
Source:Chadema blog
No comments:
Post a Comment