Pages

Thursday, May 16, 2013

Mke wa waziri Mkuu pinda afungua kongamano la Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA) jijini Arusha.

Mgeni rasmi Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda (wa tano kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi viongozi wakuu wa TAPSEA pamoja na waratibu wa Kongamano hilo la Makatibu Muhtasi  Tanzania lililofanyika leo kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa  jijini Arusha-AICC.

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Uwezeshaji na Uwekezaji,ambaye pia ni mlezi wa TAPSEA.Dkt Mary Nagu akimkabidhi zawadi ya kinyago mgeni rasmi,Mke wa Waziri Mkuu,Mh.Mama Tunu Pinda ,shoto kwake ni Mwenyekiti wa TAPSEA,Bibi Pili Mpenda wakati wa Kongamano la tatu la Makatibu Muhtasi Tanzania.

Mgeni rasmi,Mke wa Waziri Mkuu,Mh.Mama Tunu Pinda akifungua Kongamano la tatu la Makatibu Muhtasi Tanzania,lililofanyika kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa  jijini Arusha-AICC ..

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Uwezeshaji na Uwekezaji,ambaye pia ni mlezi wa TAPSEA.Dkt Mary Nagu akizungumza jambo mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye kongamano tatu la Makatibu Muhtasi Tanzania,lililofanyika kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa  jijini Arusha-AICC .

Waziri wa  Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,Mh.Sofia Simba akizungumza jambo mbele ya wageni waalikwa mbalimbali kwenye
mkutano wa Kongamano  la  tatu la Makatibu Muhtasi  Tanzania,uliofanyika mapema leo  kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa  jijini Arusha-AICC .

Sehemu ya meza kuu ndani ya mkutano wa kongamano la tatu la Makatibu Muhtasi  Tanzania lililofanyika leo kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa  jijini Arusha-AICC,kutoka kushoto ni  Waziri wa  Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,Mh.Sofia Simba,Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Uwezeshaji na Uwekezaji,ambaye pia ni mlezi wa TAPSEA.Dkt Mary Nagu,Mgeni rasmi wa Kongamano hilo la TAPSEA,Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda,Mwenyekiti wa TAPSEA,Bibi Pili Mpenda pamoja na Naibu Waziri wa katiba na sheria ambaye pia ni Mshauri wa masuala ya sheria na kazi waTAPSEA,Bi.Angella Kairuki.

Pichani ni sehemu ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye kongamano la tatu la Makatibu Muhtasi  Tanzania lililofanyika  kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa  jijini Arusha-AICC.

Picha Kwa Hisani ya Mtaa Kwa Mtaa  Blog

No comments:

Post a Comment