ALIYEMFUMANIA MKEWE GESTI AGEUZIWA KIBAO!
LILE
sakata la hivi karibuni la mwanaume aliyefahamika kwa jina la Baba Asha
kudai kumfumania mshikaji wake aitwaye Beda Mloka mkazi wa Ilala jijini
Dar es Salaam akiwa na mkewe gesti, lililoripotiwa na gazeti ndugu na
hili la Risasi Mchanganyiko, limechukua sura mpya kufuatia aliyefumania
kugeuziwa kibao na aliyedaiwa kufumaniwa.
Chanzo
chetu cha kuaminika kilichoomba jina lake lisiandikwe gazetini juzi
kililitonya Ijumaa kuwa, mara baada ya fumanizi hilo lililotokea katika
gesti iitwayo Pumzika iliyopo Msimbazi Center kisha aliyefumaniwa
kuchezea kichapo, mambo yalikwenda chinichini lakini juzikati
aliyefumania aliitwa Kituo cha Polisi, Pangani.
“Lile
tukio lilikuwa gumzo sana pale mtaani kwetu, na kwa aibu Beda alitoweka
kwa siku kadhaa lakini juzi Baba Asha akaitwa polisi, inavyoonekana
mgoni kamgeuzia kibao mwenzake
“Nilijaribu
kudadisi nikasikia Beda anadai Baba Asha na mkewe wamemchezea chezo na
anajaribu kuonesha kuwa hakufumaniwa, kitu ambacho kinawashangaza wengi
kutokana na mazingira waliyokutwa gesti,” alidai mtoa habari huyo.
Katika
kujua ukweli wa sakata hili, mwandishi wetu alimtafuta Beda bila
mafanikio lakini Baba Asha alipopatikana alisema: “Ni kweli leo
(Jumatano ya juzi) niliitwa pale Polisi Pangani, jamaa niliyemfumania na
mke wangu kaenda kunishitaki kuwa nimemfanyia mchezo.
“Kwa
kweli ni jambo la kushangaza sana, yaani kanitibulia ndoa yangu halafu
ananigeuzia kibao! Tutaona sasa yeye na mimi nani ataumbuka. Nimetakiwa
kwenda kuripoti tena pale polisi kesho (jana) na baada ya hapo nitajua
nini cha kufanya.”
chanzoL:globalpublishers
No comments:
Post a Comment