Washindi war obo fainali ya 4 timu kutoka Kenya(wenye rangi nyekundu)
na timu kutoka Ghana(wenye rangi nyeusi) wakjipongezana baada ya
kipindi kuisha
Washindi wa kwanza wa robo fainali ya mwisho ya Guinness Football
Challenge Emmanuel Okraku Kofi(kushoto) na Isaac Aryee(kulia) katika
picha ya pamoja na waendeshaji wa kipindi hicho Larry Asego na Mimi
kalinda
Timu zilizoshiriki robo fainali ya jana katika picha ya pamoja na
waendeshaji wa kipindi cha Guinness Football Challenge mara tu baada ya
kumalizika kwa kipindi hicho huku washindi wa dola 1,500 wakiwa
wamebelea pesa zao.
15 Mai 2013, Dar es Salaam jana usiku
kupitia televisheni za ITV na Clouds TV washindi kutoka Ghana katika GUINNESS®
FOOTBALL CHALLENGE walisheherekea ushindi wao wa kufuzu nusu fainali kwa
kucheza wimbo wa Azonto huku watangazaji Larry na Mimi nao wakijumuika nao.Emanuel
Okarku(27) na Isaac aryee(25) hawakufanya vizuri katika hatua ya pesa ukutani
na kupata dola za kimarekani 1,500 lakini waliufanya uwanja wote kucheza
Azonto.
Emmanuel na Isaac waliwashinda wakenya
katika hatua ya penati na kufikia hatua ya Ukuta wa pesa wa Guinness, hata hivyo timu kutoka Kenya
iliibuka mshindi wa pili na kufuzu kuingia nusu fainali.
Emmanuel, Isaac, Kenneth na Chris
pamoja na washindi wengine wa robo fainali zilizopita wataendelea kucheza na
kuziwakilisha nchi zao katika hatua ya nusu fainali na wana nafasi ya
kupeperusha bendera za mataifa yao hadi mwisho. Pia wana nafasi ya kuwa
washindi wa mashindano haya ya Pan African.
Nusu fainali hizi zitaoneshwa katika televisheni
za ITV na Clouds TV kila siku za jumatano saa 3:15 usiku ITV na saa 2:15 usiku
Clouds TV.Hakikisha haukosi kuangalia
mchezo huu wa nusu fainali.
Mashabiki na wapenzi wa soka wanaweza kupima maarifa yao
kupitia simu zao za mkononi na kushiriki GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE kupitia GUINNESS® VIP™. Jiunge bure sasa kupima maarifa yako,tembelea
m.guinnessvip.com sasa.
Usikose
kufuatilia ukurasa wetu wa facebook wa GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE kwa habari
mbalimbali.
-www.facebook.com/guinnesstanzania
Tafadhali kunywa
kistaarabu - Hairuhusiwi kwa wenye umri chini ya miaka 18.
No comments:
Post a Comment