Pages

Thursday, May 16, 2013

HEBU TUJIKUMBUSHE YA PADRI KUFUMANIWA NA MKE WA MTU!





KANISA Katoliki Jimbo la Moshi limeingia katika kashfa nzito baada ya padri wake, Father Urbanus Ngowi wa moja ya parokia zake kudaiwa kufumaniwa na mwanamke anayesemekana ni mke wa mtu, Ijumaa Wikienda lina sakata zima.
Sakata la fumanizi hilo linadaiwa kutokea Jumatatu ya wiki iliyopita chumbani kwa padri huyo, Marangu Wilaya ya Moshi  Vijijini ambako Father Ngowi inasemekana alikutwa ‘laivu’ akiwa na mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la kijamii la Mama P.
Pamoja na kunaswa huko, vyanzo havijaeleza humo chumbani wawili hao walikuwa wakifanya nini!
Habari zinadai siku ya tukio, mwanamke huyo aliingia nyumbani kwa padri huyo ambapo baadhi ya ndugu wa mumewe walikuwa wakimfuatilia baada ya madai yaliyokuwepo kwamba ana ukaribu wenye maswali mengi na mtumishi huyo wa Mungu.
“Unajua siku nyingi ilivuma kwamba Mama P na Father Ngowi wana ukaribu wenye maswali mengi, mume wake alifuatilia na kubaini ni kweli lakini akashindwa kuutenganisha ukaribu wao,” kilidai chanzo.
IJUMAA WIKIENDA NA FATHER NGOWI SASA
Baada ya kujazwa madai hayo, kama ilivyo desturi ya Magazeti ya Global Publishers likiwemo hili (Ijumaa Wikienda), lilimsaka Father Ngowi kwa udi na uvumba ambapo Ijumaa iliyopita nyakati za mchana lilifanikiwa kuzungumza naye lakini kabla ya kufanya hivyo, kifaa cha kunasia sauti kiliwekwa sawa na mambo yalikuwa hivi:
Wikienda: Haloo, naongea na Father Ngowi wa Parokia ya Korongoni, Marangu, Moshi?
Father Ngowi: Naam ni mimi, nani mwenzangu?
Wikienda: Naitwa…(mhariri anataja jina), napiga simu kutoka Magazeti ya Global Publishers.
Father Ngowi: Uko wapi?
Wikienda: Makao Makuu ya Global Publishers, Dar es Salaam.
Father Ngowi: Eeh…unasemaje?

Wikienda: Kuna madai ya wewe kukutwa na mke wa mtu chumbani. Je, unaweza kunielezea kama ni kweli na tukio lilikuwaje?
Father Ngowi: Siyo mimi.
Wikienda: Wewe siyo Father Urbanus Ngowi?
Father Ngowi: Nimekwambia siyo mimi, hao ni matapeli wanataka pesa ndiyo wametengeneza hizo picha.
Wikienda: Kwa hiyo unataka kuniambia hizi picha ni za kutengeneza?
Father Ngowi: Nimekwambia hao ni matapeli wanataka pesa.
Wikienda: Ulishaziona picha zenyewe?
Father Ngowi: Sijui.
NGOMA YATUPWA KWA MKUU WA JIMBO
Wikienda: Mbona tayari tukio hilo linadaiwa limeshafika kwenye ngazi ya jimbo, Moshi kwa Father Paul Uria?
Father Ngowi: Muulize yeye ndiye mkubwa wangu.
Wikienda: Basi nisaidie namba yake ya simu ya mkononi.
Baada ya takribani dakika 10, Father Ngowi alituma namba ya simu ya Father Uria na mambo yakawa hivi:
Wikienda (huku kinasa sauti kikiendelea kufanya kazi): Haloo…naitwa …(mhariri anajitambulisha) kutoka Magazeti ya Global Publishers, Dar es Salaam, naongea na Mkuu wa Jimbo Kanisa Katoliki, Moshi, Father Uria?
Father Uria (kwa sauti yenye unyenyekevu): Ndiyo.
Wikienda: Una taarifa za mtumishi wako, Father Ngowi kunaswa na mke wa mtu chumbani?
Father Uria: Kwanza mimi si mkuu wa jimbo, ni mwakilishi wa mkuu wa jimbo. Sipo mjini kwa sasa nipo Kilema huku vijijini kwenye huduma lakini nilikuta ‘missed calls’ zake jana (Alhamisi) kwani ilikuwa tukutane kwa sababu alishanijulisha kuwa kuna tukio kama hilo unaloniambia wewe.
NGOMA YAWA NZITO, YATUPWA LEO JUMATATU
“Kweli tulikuwa tukae jana lakini ikashindikana, leo (Ijumaa) ni sikukuu (Muungano), kesho (Jumamosi) na keshokutwa (Jumapili) ni wikiendi. Kwa hiyo tutakaa Jumatatu (leo) hivyo nipigie saa 10:00 jioni siku hiyo ili nikupe maagizo tutakayofikia na mengine.
Wikienda: Lakini Father Ngowi alikueleza tukio lilikuwaje?
Father Uria: Nimekwambia tukikaa ndiyo tutajua kilichotokea. Wewe nipigie hiyo saa 10 nikupe kitakachojiri.
Wikienda: Shukrani Father Uria kwa ushirikiano.

Kazi haikuishia hapo, Ijumaa Wikienda lilimgeukia tena Father Ngowi walau aseme kwa ufupi kilichomtokea.

No comments:

Post a Comment