Habari zilizosambaa katika mitaa ya area code +254 zinadai kuwa kundi
la hip hop lenye mafanikio makubwa nchini Kenya, Camp Mulla limempiga
chini first lady na lead singer wa kundi hilo, Miss Karun kutokana na skendo zinazomkabili
Kwa mujibu wa maneno ya mtaani inasemekana nafasi ya Miss Karun
itachukuliwa na mrembo mwingine aitwaye Tiri, ambaye ni mpenzi wa member
na producer wa kundi hilo K’cous.
Siku chache zilizopita kulizuka uvumi wa uwezekano wa members wa
kundi hilo kuendelea na solo projects kwa kila mmoja wao ifikapo mwezi
June 2013, kitu ambacho kinafanya tetesi za Miss Karun kuondolewa
kundini kuchukuliwa kama dalili za kuvunjika kwa kundi hilo.
Camp Mulla wanategemea kupanda kwenye jukwaa moja na Snoop Lion
katika concert ya MTV all stars Kwa Zulu-Natal hivi karibuni nchini
Africa Kusini, show ambayo watampandisha mrithi wa Miss Karun kwa mara
ya kwanza.
No comments:
Post a Comment