Pages

Thursday, May 16, 2013

BREAKING NEWS: Linah, Barnaba kutupiwa vilago THT?


Msanii Linah 

Barnaba

 

KUELEKEA shoo maalumu ya Miaka 13, ya mwanamuziki nguli wa bongo fleva nchini na kiongozi wa bendi yenye msisimko mkubwa ya ‘Machozi Band’, Judith Wambura ‘Lady Jay Dee’ au Jide’  huenda kwa upande wa wasanii wa Nyumba ya Vipaji ya THT, Linah Sanga na Barnaba  mwaka huu ukawa mchungu kwao kufuatia kuwepo taarifa za kutimuliwa na uongozi wa juu.

 

Kwa mujibu wa vyanzo kutoka kwa mtu wa karibu wa Linah kilieleza kuwa mpaka sasa msanii huyo hana raha na wala hajui ataanza vipi katika harakati zake za kimuziki hasa kufuatia hivi karibuni kukacha shoo ya nguli Lady Jay Dee kwa shinikizo kutoka kwa wakubwa zake.

 

Hata hivyo, Linah inadaiwa uongozi wa juu umekaa kikao na hatua iliyofuatia kwenye kikao hicho ni kuwaondoa kabisa kwani huenda wakatia doa wasanii wenzao ndani ya kundi hilo.

 

“Juzi Lina,haikuwa kawaida yake maana hata alipopigiwa simu na ** kwa ajili ya hatua zingine alionekana kuw na hofu, na wala hakutaka kusikia ushauri wangu ambao nilikuwa nikimhusia kuwa aachane na mawazo hayo kwani jambo analoliwaza huenda likaisha na hata maamuzi yatakayotoka yatakuwa ni kawaida” kilieleza chanzo kutoka kwa mtu wakaribu wa Lina, amabaye hata hivyo alisema kuwa huenda ukweli wa jambo ukawa hadharani.

 

Hata hivyo taarifa za ndani za uongozi wa THT zilibainisha kuwa mpango wao wa kuwashughulikia wasanii hao upo pale pale na taratibu zinafuata ili zisilete madhara kwa wasanii waliopo ndani ya THT  na watu wa karibu wanaoiunga THT.

 

“Wewe nani kakwambia kama tumewaadhibu Lina na Barnaba?, ndio kwanza tunakusikia wewe hizo taarifa,  sisi tunafanya mambo yetu wao waache wafanye yao tukiwa nao sie na tunao uwezo wa kuwatimua ilikulinda hadhi ya THT” Kilieleza chanzo hicho ambacho hata hivyo kutokana na usalama wa jina lake tumelihifadhi. Ambapo namba yake inaishia na**08.

 

Aidha, katika ‘ku-balance’ huondo kamili wa habari hizi wasanii hao wote walipotafutwa kwenye simu zao za mkononi lakini hawakuweza kuwa hewani kwa muda mrefu.. na hata alipopigiwa mtu wao huyo wa karibu naye alizima simu.

 

Katika kile kinachoeleza kupamba moto shoo hiyo, na kujaa kwa taarifa mbalimbali juu ya wasanii watakaopamba shoo ya miaka 13, Mei 31 ndani ya Nyumbani Lounge, Tayari tiketi zimeanza kuuzwa maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Saalam.

 

Shoo hiyo ya kijanja Nyumbani Lounge, patakuwa hapatoshi pale wadau wa burudani na wastaarabu wote watakapojumuika kwa pamoja ku-shoo love kwa Lady Jay Dee  na Machozi Band, huku listi ya mastaa mbalimbali wanatarajia kuudhuria sambamba na ‘surprise’ kutoka kwa mastaa hao ambao kwa sasa wengi wapo kimya wakihofia kutengwa na wazee wa ‘fitina bin Logiki’.

Awali kulikuwapo na taarifa za kuwapo kwa msanii Matonya, ambaye hata hivyo mtandao wa Lady Jay Dee ulitoa hadharani kuwa mwanamuziki huyo ameshachukua ‘advance’ ya shoo hiyo na wazee wa ‘kuingilia logik’ wameshamtisha Matonya ili ajitoe, lakini akiwa ameshatafuna pesa ya watu.

 

Mtandao huo wa kijamii  blog, ilinukuu kila kitu juu ya Makubaliano baina ya Capt.Gadna G Habashi na Matonya ambapo pia unaweza kuyasoma kupitia (Ladyjaydee.blogspot.com) Pia ulitoa kwa mara ya kwanza picha,maelezo muhimu na video ya wanamuziki hao wawili Linah na Barnaba wakiingia mkataba wa shoo hiyo na pia kuhamasisha watu kufika Mei 13..

 

**KWA TAARIFA ZAIDI  KWA KINA JUU YA BARNABA NA LINAH, usikose kuzisoma katika gazeti la Tanzan ** Pindi watakapopatikana tutaweka hadharani kila kitu.

Mwisho

No comments:

Post a Comment