POLISI AKUTWA AMEKUFA
ASKARI Polisi E7122 George Elias Mwakani, aliyekuwa akifanya
kazi mjini Musoma, Mara, amekutwa amekufa katika eneo la mtaa wa Nyasura
huku mwili wake ukiwa na majeraha.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Absalom Mwakyoma, alisema askari huyo
aliyekuwa na cheo cha Koplo, alitoweka kazini tangu Aprili 30 mwaka huu
na kwamba tayari walikuwa wameshasambaza taarifa za kupotea kwake
katika maeneo mbalimbali.
“Askari huyo alitoweka tangu Aprili 30 mwaka huu na tulikuwa
tumeshatoa taarifa hadi jana nilipopata taarifa za kifo chake lakini
tunaendelea kufanya uchunguzi wa kifo chake,’’ alisema.
Akizungumza na Tanzania Daima, mdogo wa marehemu, Abel Elias, alisema
kaka yake alionana naye mara ya mwisho mwezi uliopita akiwa kazini
kwake.
Mwili wa askari huyo umehifadhiwa katika hospitali ya DDH Bunda
ukisubiri kufanyiwa uchunguzi na madaktri ambao watatoa taarifa sahihi
ya kifo hicho.
Source:Tanzania daima
No comments:
Post a Comment