G. Lema: “Serikali huwezi kutibu Malaria kwa kumpa Mgonjwa Panadol”
“Serikali huwezi kutibu Malaria kwa kumpa Mgonjwa Panadol” - G. LemaNimefuatilia leo asubuhi juu ya maneno niliyotamka Olasiti Kanisani baada ya bomu , nimeona michango mbali mbali katika mitandao ya jamii , nawapongeza wale wenye kutambua ukweli na kuutetea ukweli lakini pia wale wasiojua ukweli lakini wamefanikiwa kupata maarifa ya kujua matumizi ya kompyuta kwa hiyo nakusikia fahari kuandika maoni yeyote wanayotaka , Watu hawa ni muhimu kwani wanasaidia kutambua kwa wepesi kuwa sio kila mtu anayeweza kutumia Internet ni mwenye uelewa na akili , hivyo inasaidia Wazazi kujua namna ya kusaidia watoto wao katika siku zijazo.
Maneno niliyotamka ni muhimu sana , NUKUU , “ Nawapa pole wote mliofikwa na majanga haya , Mimi nichukue fursa hii kuwapa pole , lakini niwe jasiri sana kusema ukweli kama ninyi waandishi wa habari hamtafanya editing…..
“ Kwanza kabisa niweke wazi kuwa jambo hili limesababishwa na chokochoko za udini ambazo muasisi wake ni Serikali ya CCM na viongozi wake, aliyepiga bomu hapa leo siyo jambazi wa kutaka mali bali ni mtu aliyeelewa na kufundishwa tofauti kwa nia mbaya kuhusu dini nyingine, haya maneno ya udini yalianzishwa na viongozi wa Chama tawala lengo likiwa ni kuwagawa na kuwatawala raia lakini kwa sasa wamelikoroga, wamewachonganisha watu wa dini mbalimbali hasa Waislam na wakristo ambao ndio wengi katika taifa hili bila kujua madhara ya mkakati huu kuwa utaligawa Taifa.
Sasa basi kazi hiyo waliyoifanya haya ndio mavuno yake kwani tukio hili lina sura zote za kiimani na kigaidi na nilitake jeshi la polisi kufanya kazi ya kuwakamata haraka kama ambavyo walinikamata mimi nyumbani kwangu kwa mabomu na vitisho , nawapa pole sana watu wote mliopatwa na janga hili .
No comments:
Post a Comment