HABARI,MATUKIO,MICHEZO,MATANGAZO NA BURUDANI. Wasiliana moja kwa moja kupitia icehabari@gmail.com
Thursday, May 9, 2013
Mikasa ya Kuvunjika Kwa Ndoa Ambayo Huwezi Kuamini
Sababu mbalimbali huchangia kuvunjika kwa ndoa. Kukosa maelewano katika ndoa na kokosekana kwa uaminifu ni miongoni mwa sababu kubwa ambazo huvunja ndoa za watu wengi.
Leo Nifahamishe tunawaletea baadhi ya sababu zilizopelekea kuvunjika kwa ndoa hizi. Unaweza usiamini ukisikia sababu hizo.
MKASA NAMBA 1: Mume Aliyemwacha Mkewe Ambaye Alikuwa Akiona Aibu Kufanya Mapenzi Kwa Mwaka mzima wa ndoa yao.
Mahakama ya mji wa Tainan, Taiwan ilikubali ombi la mume kuvunja ndoa yake na mkewe ambaye alikuwa akiona aibu kufanya tendo la ndoa kwa kipindi cha mwaka mmoja cha ndoa yao.
Mwanaume huyo aliyejulikana kwa jina la pili kama Chen, 38, alikutana na mpenzi wake ambaye baadae aliamua kumuoa, Lin, 29, kwenye internet kwenye mtandao wa matchmaker.
Baada ya kutongozana kwa miezi mitatu, hatimaye waliamua kuoana, lakini Lin aligoma kufanya mapenzi kwakuwa alikuwa anaona aibu kumvulia nguo mumewe.
Usiku wa harusi yao, Lin alilala na shela lake la harusi na wakati Chen alipojaribu kulala naye alimsukuma na kumwambia "Wewe ni mpuuzi, toka hapa" na siku iliyofuatia aliondoka na kurudi kwa wazazi wake.
Hali hiyo iliendelea wa mwaka mzima Lin akiendelea kumnyima unyumba Chen huku akilala naye kitanda tofauti.
Jaji aliivunja ndoa hiyo na kusema ni ajabu Lin kumnyima unyumba mumewe kwa mwaka mzima.
Jaji huyo pia alimtaka Lin amlipe fidia Chen ya nyumba aliyonunuliwa, arudishe mahari aliyotolewa kwakuwa alikuwa hampi unyumba mumewe.
MKASA NAMBA 2: Ndoa Iliyovunjika Baada ya Uume Kuvunjika Wakati wa Tendo la Ndoa.
Mwanaume mmoja wa nchini Urusi alikimbiwa na mkewe baada ya kipande kilichoongezwa na madaktari kuufanya uume wake uwe mrefu kuvunjika katikati ya mchezo.
Grigory Toporov, 47, aliwaambia madaktari kwamba anashindwa kumfikisha mkewe kileleni kwa hiyo alitaka uume wake uongezwe urefu.
Madaktari walimtengenezea kipande maalumu cha uume wa bandia kilichoongezwa kwenye uume wake kuufanya uwe mrefu.
Hata hivyo uume huo ulivunjika wakati akitumia. Alimwambia mkewe kuwa atatengeneza tena lakini mkewe alimwambia "nimechoka na uchovu wako kitandani, naomba talaka".
MKASA NAMBA 3: Ndoa ya Miaka 60 yavunjika baada ya Babu wa Miaka 81 kufumaniwa
Bibi mmoja wa nchini Ujerumani, aliivunja ndoa yake na mumewe mwenye umri wa miaka 81 baada ya kumfumania akila uroda na mfanyakazi wake kazini kwake.
Georg Meister na kimada wake huyo ambaye alikuwa amemzidi miaka 30 walikuwa wakifanya kazi sehemu moja, walikuwa kwenye mapenzi ya siri mpaka siku walipofumaniwa wakila uroda ndani ya ofisi baada ya kusahau kushusha mapazia.
Mke wa Georg, Ruth baada ya kusikia fumanizi hilo alimfukuza kwenye nyumba Georg na aliomba talaka na kisha alimvuta ndani mpenzi wake kijana aliyekuwa akiishi mlango wa tatu kutoka kwenye nyumba yao.
MKASA NAMBA 4: Amwacha Mkewe Baada ya Kugundua Alimdanganya Umri wake
Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Luo, alimdanganya mumewe umri wake na alipewa talaka baada ya miaka 10 ya ndoa baada ya mumewe kugundua umri halisi.
Luo alikuwa na umri wa miaka 30 wakati mumewe alipomchumbia, lakini alimwongopea kuwa ana umri wa miaka 24.
Mwaka 2007, mumewe aligundua uongo huo na kuamua kuvunja ndoa yao ya miaka 10.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment