Pages

Thursday, May 9, 2013

KIBARUA WA TANESCO IRINGA ALIYENASA KTK NYAYA WAKATI AKIWA KAZINI AFARIKI DUNIA


 


 Kibarua  wa  wa Shirika la Umeme Tanesco mkoani Iringa, Selemani Mbuma (pichani)mkazi wa Isoka mjini Iringa ambae  alinasa  katika nyaya  za umeme wakati akiwa kazini  baada ya wenzake kuwasha umeme afariki  dunia  leo 

Kijana  huyo  alinasa katika  umeme miezi miwili  iliyopita akiwa  juu ya nyaya  za umeme akiendelea na ufundi eneo la Mlandege kabla ya  wenzake kuwasha umeme kimakosa wakati akiendelea na matengenezo na  kupelekea  kuungua  vibaya  mwilini .

Kijana  Mbuma amefariki  dunia mapema  leo akiwa katika Hospitali ya  Rufaa ya  mkoa wa Iringa ambako alikuwa akipatiwa matibabu na mwili  wake unatarajiwa kuzikwa  kesho .


Kifo   cha  kijana  huyo  kimeibua maswali  mengi  zaidi kutoka kwa  vibarua  wenzake na  wamelitaka  shirika  hilo la Tanesco  kuacha kuendelea  kuwatumikisha  vijana  hao kwa maslahi  duni ya chini ya Tsh.6000 kwa  siku  wakati  kazi kubwa  imekuwa ikifanywa na  vibarua hao huku  wafanyakazi ambao  wanalipwa kila mwezi hukaa maofisini  bila kazi.


Tanesco  Iringa imekuwa ikilalamikiwa kutokana na tatizo la kunaswa kwa kibarua  huyo katika nyanya za umeme na moja kati ya maswali  ni pamoja na hili hivi hakuna  hawawasiliani pindi wanapotaka kurudisha umeme huo? au hakuna fundi in charge ambaye ndio kiongozi wa msafara wa ufundi ambaye ndie atakaye husika na miongozo yote ya kuhakikisha kuwa hakuna mtu anaye endelea na matengenezo ndio umeme uwashwe? 

jibu naweza jipa mwenyewe kuwa lazima awepo ila ni Ufanyaji kazi wa mazoea na kuwaamini sana hawa wanaoitwa saidia kuwapa majukumu yaliyokuwa makubwa kuliko uwezo wao na ndio makosa kama haya yanatokea, maisha ya mtu yanapotea kwa uzembe  kama huu.

Jambo jingine ambalo  waweza  kujiuliza kwanini fundi anafanya kazi  bila kuvaa hata Groves mkononi wala mavazi ya kazi?.

Source francis Godwin.

No comments:

Post a Comment