Pages

Wednesday, May 8, 2013

MAUA SAMA MOTO UWAKAO KASI KATIKA KIZAZI KIPYA


 



Maua Sama ni msanii chipukizi kutoka Moshi. Ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo Cha Ushirika na Biashara Moshi.

Maua ni almasi mchangani ambayo imegunduliwa na MwanaFA baada ya kupata ‘demo’ yake aliyofanyia studio za Moshi na kuipeleka mbele ya “Management Team” yake Lifeline/T.I.A ambao moja kwa moja wakamchukua.




Maua anafanya kazi chini ya uangalizi wa Lifeline/T.I.A Inc; Label ya muziki ambayo inasimamia kazi za muziki za MwanaFA.So Crazy ambao ni wake wa kwanza umetayarishwa na producer Marco Chali wa MJ Records na amemshirikisha MwanaFA.




Mipango iliyopo ni kumfanya Maua Sama kuwa mwimbaji bora wa muziki Tanzania.



Huyu ndiye Maua Sama mwanmuziki chipukizi anayefanya vyema na single yake "SOO CRAZY"


1 comment: