Pages

Sunday, May 12, 2013

Mwenyekiti wa wakulima kizimbani, anunua pamba bia leseni

Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima wa Pamba Tanzania (Tacoga), Elias Zizi amepandishwa kizimbani kwa kosa la kuhujumu kilimo cha zao.
Zizi anashtakiwa kwa kununua pamba kabla ya musimu, ikiwamo kufanya biashara ya pamba bila leseni.
Mwendesha Mashtaka Polisi, Clement Kitundu alidaiwa mahakamani hapo kuwa mshtakiwa alikamatwa Mai 6, mwaka huu Kijiji cha Mbiti, Kata ya Mango, wilayani Bariadi, Mkoa wa Simiyu akinunua pamba.
Kitundu alidai kuwa suala hilo ni kosa tena bila leseni. Ilidaiwa kuwa kwa vipindi na siku tofauti, mshtakiwa ambaye ni kiongozi wa chama cha wakulima anayetambua na kuelewa sheria na kanuni, alitenda kosa hilo na kufanikiwa kununua zaidi ya tani moja ya pamba kwa nia ya kuiuza baadaye.
Mshtakiwa alikana mashtaka hayo na kuachiwa kwa dhamana, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya Bariadi, Robert Oguda aliamua mahakama kuhamia eneo la tukio kupima na kushuhudia pamba hiyo ikiwamo kupima uzito, kazi iliyofanyika chini ya usimamizi wa polisi.

No comments:

Post a Comment