Taarifa hiyo ni sehemu ya matokeo ya uchunguzi
unaofanywa kutokana na tukio hilo lililotokea Jumapili iliyopita,
kupoteza maisha ya watu watatu na kujeruhi wengine 67 baadhi wakiwa
katika hali mbaya.
Polisi nchini kwa kushirikiana na vyombo vingine
vya dola na Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) vipo katika uchunguzi
kuhusu tukio hilo lililotokea muda mfupi kabla ya kanisa hilo
kuzinduliwa rasmi ambapo mgeni rasmi alikuwa Balozi wa Vatican nchini
Askofu Mkuu Francisco Padilla.
Akizungumza na gazeti hili jana, Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Arusha, Lebaratus Sabas alisema kuwa uchunguzi umebaini kuwa
bomu hilo siyo la kutengenezwa kienyeji, bali ni la kiwandani.
“Uchunguzi wa awali unaonyesha, bomu lililotupwa
kanisani siyo la kutengeneza kienyeji. Hii ni kwa mujibu wa taarifa
tulizozipata kutoka kwa wataalamu ndani ya Jeshi la Polisi,” alisema na
kuongeza:
“Taarifa kamili itatolewa Jumatatu (kesho) kwa
kuwa kuna baadhi ya watuhumiwa wanaendelea kukamatwa na kuhojiwa na
polisi na wengine watafikishwa mahakamani.”
Kamanda Sabas alisisitiza kuwa Jeshi la Polisi
linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na halitasita kutoa taarifa kwa
umma kukiwa na haja ya kufanya hivyo, ambapo amewaomba wote wenye
taarifa zinazoweza kusaidia upelelezi kuzitoa polisi.
Arusha na Ugaidi
Taarifa hizo zimekuja huku mji wa Arusha ukianza kuingia katika rekodi mbaya ya kuhusishwa na vitendo vya ugaidi, baada ya matukio matatu kuuhusisha mji huo wa kitalii nchini.
Taarifa hizo zimekuja huku mji wa Arusha ukianza kuingia katika rekodi mbaya ya kuhusishwa na vitendo vya ugaidi, baada ya matukio matatu kuuhusisha mji huo wa kitalii nchini.
Kuhusishwa kwa mji huo na ugaidi kunatokana na
wahusika wakuu wa milipuko iliyotokea nchini na nchi jirani kudaiwa
kwamba waliratibu vitendo hivyo wakiwa katika mji huo.
Taarifa zilizopo zinaonyesha kuwa mwaka 1998
mtuhumiwa mkubwa wa ugaidi, Ahmed Khalfan Ghailani, alidaiwa kukaa kwa
muda mjini Arusha na kununua baruti za kulipulia miamba kutoka kwa
baadhi ya wachimbaji wa madini ya Tanzanite Mirerani, Wilaya ya
Simanjiro.
Baadaye ilibainika kuwa mabomu yaliyotumika
kulipua Ofisi za Ubalozi wa Marekani katika miji ya Dar es Salaam na
Nairobi nchini Kenya katika tukio la Agosti 7, mwaka huo wa 1998,
malighafi zake zilinunuliwa mkoani Arusha na Ghailani.
Katika tukio jingine la mwaka 2011, wakazi wawili
wa Arusha, Abdulmalik Majid na Hija Seleman Nyandondo (30), walikamatwa
kwa tuhuma za kushiriki njama za kuilipua kwa bomu klabu moja ya usiku
katika Jiji la Kampala nchini Uganda lililopoteza maisha ya watu 74,
waliokuwa wakitazama mpira wa Fainali za Kombe la Dunia, mwaka 2010.
No comments:
Post a Comment