Mabingwa watetezi, Madrid walihitaji
ushindi nyumbani kwa wapinzani wa Jiji wa Barca kuendelea kumsubirisha
kocha Tito Vilanova na vijana wake kusherehekea ubingwa, lakini
wakalazimishwa sare ya 1-1.
Matokeo hayo yanaifanya Barca iongoze La
Liga kwa pointi saba zaidi wakijiandaa kucheza na Atletico Madrid leo,
huku kikosi cha Jose Mourinho kikiwa kimebakiza mechi mbili kumaliza
msimu wa ligi.
Super sub: Cristiano Ronaldo alitokea benchi na kuisawazishia Real Madrid
Kaka wa Real Madrid akiwatoka watu
Mashabiki wa Barcelona wakishangilia jana taji la La Liga baada ya Real Madrid kuchemsha
Hii ni mara ya nne katika miaka mitano
Barca kutwaa taji hilo na mara ya 22 kwa ujumla - wakizidiwa mara 10 na
wapinzani wao wa jadi, Madrid.
Na pia ni taji la kwanza kwa kwa Barca
chini ya kocha mpya Vilanova, ambaye alifungwa na Madrid katika kuwania
Super Cup ya Hispania mwanzoni mwa msimu na kutolewa katika Nusu Fainali
ya Ligi ya Mabingwa na Bayern Munich na Kombe la Mfalme dhidi ya
Madrid.
Vilanova, ambaye wiki hii alirejea New
York alikokuwa anatibiwa saratani kwa miezi miwili mapema mwaka huu,
alipandishwa kutoka timu ya vijana kurithi mikoba ya Pep Guardiola
aliyeondoka mwishoni mwa msimu uliopita.
Benchi la Real Madrid
Walipumzishwa: Ronaldo, Iker Casillas na Karim Benzema benchi
Espanyol, walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Christian Stuani dakika ya 23 na Hector
Moreno alifunga bao ambalo lilikataliwa wakati Real ina nafasi ya
kutwaa taji moja, itakapomenyana na Atletico Madrid katika Fainali ya
Kombe la Mfalme Ijumaa.
Hata hivyo, Cristiano Ronaldo alitokea benchi na kusawazisha dakika ya 58 kufuatia kazi nzuri ya Gonzalo Higuain.
Espanyol ilipoteza mchezaji mmoja dakika
za majeruhi wakati Victor Sanchez alipoonyeshwa kadi ya pili ya njano
baada ya kumchezea rafu Higuain, lakiini mpira wa adhabu uliopigwa na
Ronaldo ulipaa.
No comments:
Post a Comment