Wiki hii imeendelea kuwa mbaya kwa mashabiki wa Manchester United, siku chache baada ya Sir Alex Ferguson kutangaza kustaafu, leo hii kiungo wa timu hiyo Paul Scholes nae ameamua kumfuata kocha wake kwa kutundika daluga kuitumikia klabu yake pekee katika soka la kulipwa.
Gwiji
huyo wa Manchester United mwanzoni alistaafu wakati wa mwisho mwa msimu
wa 2010/2011, lakini akaamua kubadili maamuzi na kurejea kwenye timu
mwezi January mwaka jana.
Katika taarifa yake Scholes, 38, alisema:Hatimaye ninatundika daluga zangu kabisa!
"Kucheza soka ndio ilikuwa kila kitu kwangu, na kuwa na mafanikio kwa
muda mrefu kwenye soka ndani ya Manchester United, chini ya meneja bora
kabisa wa muda wote, ni heshima kubwa.
“Timu ipo kwenye hali nzuri na itaendelea kufanikiwa chini ya uongozi wa David Moyes.”
Scholes
amecheza zaidi ya mechi 700 akiwa na jezi ya United na kesho atakusanya
medali yake ya 11 ya kombe la premier league watakapocheza dhidi ya
Swansea.
No comments:
Post a Comment