Kikosi Cha Bongo Movie ambacho kimewatoa Jasho Taswa Fc
Kikosi cha Taswa FC
kilichoshikishwa Kamera na timu ya bongo movie hapo jana katika bonanza
la taswa na bongo movie lililofanyika katika viwanja vya TCC Chang'ombe
ambapo Bongo Movie ilishinda magoli 2 kwa 0 dhidi ya Taswa fc
Mchezaji wa Taswa FC ambaye pia
ndio mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari Za Michezo Juma Pinto
(Mwenye Jezi ya Blue no 16) akigombania mpira dhidi ya Mchezaji wa Bongo
movie katika mechi ya kirafiki iliyofanyika jana katika uwanja wa TCC
Chang'ombe ambapo bongo movie iliibuka na ushindi wa Magoli 2 kwa 0
Mchezaji wa bongo movie Steve
Nyerere akikimbilia mpira katika mechi ya kirafiki kati ya bongo movie
na Taswa Fc iliyofanyika jana katika uwanja wa TCC Chang'ombe, bongo
movie iliibuka mshindi kwa magoli 2 kwa 0 dhidi ya taswa fc.
hatari langoni mwa timu ya Taswa Fc.
Refarii wa Mechi kati ya Bongo
Movie na Taswa Fc ambaye ni msanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Kiba
akiwa makini kufuatilia Mchezo huo wakati mtanange ukiendelea...Refa
hapo unafanya nini sasa....
Mchezaji wa bongo movie akijaribu
kumtoka beki wa Taswa Fc katika mechi ya kirafiki dhidi ya Taswa Fc
ambapo bongo movie ilishinda magoli 2 kwa 0.
Kipa wa taswa fc alipokuwa
akijaribu kuokoa mchomo bila mafanikio na kupelekea Bongo movie kuandika
goli la kwanza kwa mkwaju safi.
Wachezaji wa Bongo movie wakiwania
mpira dhidi ya mchezaji wa Taswa FC jana katika mechi ya kirafiki
iliyofanyika katika uwanja wa TCC Chang'ombe
Timu ya Bongo Movie ikichuana
vikali katika mchezo wa mpira wa pete dhidi ya timu ya taswa queen
ambapo kwenye mchezo huu bongo movie walichezea kichapo cha zaidi ya
magoli 50
Mchezaji wa Bongo Movie akijaribu
bahati yake ya kushinda goli dhidi ya Taswa queen katika mechi ya
kirafiki iliyofanyika jana katika uwanja wa TCC Chang'ombe katika mchezo
wa netball bongo movie walipokea kichapo kizito kutoka kwa Taswa queen.
Mchezaji wa Bongo Movie Jackline
Wolper akijiandaa kuingia kwaajili ya kuisaidia timu yake ambayo
ilipokea kichapo kizito kutoka kwa waandishi wakike wa habari za michezo
taswa queen katika mchezo wa kirafiki uliofanyika jana katika uwanja wa
TCC Chang'ombe Temeke.
Baadhi ya waandishi wa habari
wakifuatilia mchezo wa netball kwa makiini wakati timu yao ikichuana na
timu ya bongo movie katika mechi ya kirafiki iliyofanyika katika uwanja
wa TCC Chnag'ombe ambapo Taswa queen waliibuka kwa ushindi mzito dhidi
ya bongo movie.
Baadhi ya mashabiki na waigizaji
wa filamu za kibongo wakifuatilia mtanange wa mpira wa miguu aka soccer
wakati timu ya mpira wa miguu ya bongo ikichuana vikali na timu ya mpira
wa miguu ya waandishi wa habari za michezo aka Taswa fc katika mchezo
wa kirafiki uliofanyika katika uwanja wa TCC Chang'ombe hapo jana na
kupelekea bongo movie kuibuka vinara kwa kuichapa taswa fc magoli 2 kwa
0.
Baadhi ya wadau wa michezo
wakifuatilia mtanange wa mpira wa miguu kati ya bongo movie na taswa fc
uliofanyika jana katika viwanja vya TCC Chang'ombe na bongo movie
kuibuka washindi kwa magoli 2 kwa 0
Bloggerz
wakiwa bize katika kumuzisha matukio. Kutoka Kushoto ni Othman Michuzi
wa Mtaa kwa Mtaa blog, Le Mutuz William Malechela, Mwenyekiti wa Chama
Cha Waandishi wa habari za Michezo TASWA Mh Juma Pinto, Muhidini Sufian
wa Sufiani Mafoto Blog, akifuatiwa na Bepari aka Lukaza the Blogger wa
Lukaza Blog wakiwajibika.
No comments:
Post a Comment