Afande Kenyela
Hali ya taharuki ililikumba Jiji la Dar es Salaam jana baada ya
kuwapo kwa taarifa za kulipuliwa kwa bomu katika Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kunduchi Mtongani, Manispaa ya
Kinondoni.
Taarifa hizo zilisambaa katika mitandao ya kijamii
na baadhi ya vyombo vya habari na kuwafanya wananchi kujiuliza nini
kinalikumba taifa katika kipindi hiki.
Hali hiyo ya taharuki na mshtuko kwa wananchi
inatokana na shambulio la bomu katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu
Joseph Mfanyakazi la Parokia ya Olasit jijini Arusha, lililotokea
Jumapili
iliyopita na kusababisha vifo vya watu watatu na majeruhi 67.
Hata hivyo, taharuki ya jana ilisababishwa na
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni kufyatua mabomu ya machozi walipokuwa
wakitekeleza operesheni ya kukamata wahalifu waliokuwa katika majengo
mawili mali ya Kanisa la KKKT, Kunduchi Mtongani.
iliyopita na kusababisha vifo vya watu watatu na majeruhi 67.
Hata
hivyo, taharuki ya jana ilisababishwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa
Kinondoni kufyatua mabomu ya machozi walipokuwa wakitekeleza operesheni
ya kukamata wahalifu waliokuwa katika majengo mawili mali ya Kanisa la
KKKT, Kunduchi Mtongani.
Katika kutekeleza operesheni hiyo polisi hao
walifunga njia zote tatu za kutoka na kuingia eneo hilo ili kuhakikisha
vibaka hao hawakimbii.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Samweli
Nzuna alisema kuwa baada ya kuona wanakaribia eneo hilo, polisi
walifyatua juu mabomu ya machozi yaliyotoa mlio mkubwa ili kuwachanganya
wahalifu waliokuwa katika majengo hayo ya kanisa wakicheza kamari na
kuvuta bangi .
Alisema mara baada ya polisi hao kufyatua mabomu
hayo wananchi waliokuwa karibu na eneo walianza kukimbia ovyo wakidhani
jengo la kanisa limelipuliwa na vibaka hao walikimbia kuelekea katika
mikoko iliyo mkabala na kanisa kabla ya polisi kufyatua tena bomu la
machozi ili kuwazuia vibaka hao kukimbia zaidi.
“Wakati wa utekelezaji wa operesheni hiyo hakuna
mwananchi yeyote aliyeumia ila walishtuka na wengine kudhani kuwa kanisa
lilikuwa limelipuliwa kwa bomu na wahalifu, kwani awali hawakujua kama
waliofanya hivyo ni polisi,”alisema Nzuna.
Naye Aloys Mwamanga, mkazi wa eneo hilo ambaye pia
ni Rais wa Shirikisho la Wenye Viwanda na Kilimo nchini (TCCIA),
alisifu operesheni hiyo akisema:
“Vibaka hawa wamekuwa wakisumbua kwa kipindi
kirefu eneo hili, wameniibia hata runinga yangu hivyo naona hivi sasa
amani itarejea eneo hili.”
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni,
Charles Kenyela alikiri tukio hilo akisema kuwa kwa sasa jeshi lake
linaendesha operesheni kali ya kuwasaka wahalifu wote.
“Hivi sasa tupo katika kipindi kigumu ukilinganisha na tukio lililotokea Arusha.
Source: Mwananchi.
No comments:
Post a Comment