Kamanda wa Polisi Kinondoni, Charles Kenyela
Wanafunzi wa Sekondari ya Kata ya Manzese, wamedai kutokewa na
hali isiyoeleweka na kusababisha wenzao 32 kuanguka na kupoteza fahamu
kwa nyakati tofauti.
Tukio hilo lilianza saa 2:35 asubuhi na kudumu
hadi saa 6:00 mchana. Kutokana na hali hiyo, uongozi wa shule hiyo
umesitisha masomo kutwa nzima ya jana ili kuwahudumia wanafunzi hao na
kuwaruhusu wengine kurudi nyumbani hadi kesho.
Mkuu wa sekondari hiyo alipofuatwa ofisini kwake
kuzungumzia suala hilo, alikutwa akiombewa na Mchungaji wa Kanisa la
Tanzania Assemblies of God (TAG), ambaye baadaye alijitambulisha kwa
jina la Godfrey Alphonce maarufu kama Punda wa Yesu.
Mchungaji huyo baada ya kumaliza ibada hiyo, Mkuu
wa shule alitoka akiwa ameambatana na watu wengine na alikataa
kuzungumza na waandishi wa habari waliokuwapo.
“Nimechanganyikiwa naomba uniache, akili yangu haipo vizuri,” alisema mwalimu huyo na kupanda gari kisha kuondoka eneo hilo.
Kamanda wa Polisi Kinondoni, Charles Kenyela alipulizwa kuhusiana tukio hilo, alisema ofisi yake haijapata taarifa.
No comments:
Post a Comment